'Ukiendelea kuwa na hiyo roho chafu utajinyonga,' Bahati amwambia shabiki baada ya kusema haya

Muhtasari
  • Bahati ampa shabiki bonge la jibu baada ya kumkejeli
  • 'Ukiendelea kuwa na hiyo roho chafu utajinyonga,' Bahati amwambia shabiki baada ya kusema haya
  • Kwa siku chache msanii huyo amekuwa kwenye vichwa vya habari kwa maisha ambayo anaishi na mewe Diana Marua
bahati1__1570190817_94158
bahati1__1570190817_94158

Msanii Bahati amemnyamazisha na kumjibu shabiki wake ambaye alijaribu kuwakosoa na kuwakejeli baada ya kuposti picha kwenye mitandao ya kijamii.

Baada ya Bahati kuposti picha hiyo aliandika ujumbe mfupi wa maneno ya kibao chake cha 'Wanani'.

"Twende Nyumbani Tukamuone Aunty... Nawenye Wivu Tuwaite Harusini.Kama Uhai angepewa Mummy,Angefurahi Kukuona Hunny. ❤️#Wanani Wedding Loading. ....... %." Bahati Aliandika.

Kwa muda usio kuwa mefu shabiki huyo aliwauliza kwanini wanaringa ilhali hawana chochote cha kuringa.

Huu hapa ujumbe wa shabiki huyo;

"Wivu ya nini sasa....nini cha muhimu au cha maana ambacho mo nacho???"

Ni vita ambavyo vimeshuhudiwa kati ya Bahati na shabiki huyo huku Bahati akimpa bonge la jibu.

"@Catherine_Maina_Kanyi, kwanza tuna nyuso ambazo tunajivunia kuziposti. Nashindwa unakaa aje kama ukona na zero posts. Ukiendelea kukaa na hiyo roho chafu hivyo soon Utajinyonga akii." Alijibu Bahati.

Awali Bahati amekuwa  kwenye vichwa vya habari baada ya kumpeleka Diana kujivinjari na hata kumpa zawadi tele.