Diamond amlimbikizia sifa baby mama Zari Hassan

Muhtasari
  • Diamond asema kati ya baby mama wake zari ndiye bora kulea wanawe 
  • Msanii huyo alisema kwamba hana uhusiano wowote na Zari 
Diamond Zari
Diamond Zari

Staa wa bongo Diamond Platnumz kwenye mahojiano alizungumzia mambo kadha wa kadha kuhusu maisha yake akiwemo baby mama wake Zari Hassan.

Diamond alikuwa ameenda kwenye studio za wasafi fm kuzindua kibao chake kipya huku 'Waah' akimshirikisha msanii wa  Rhumba  Koffi Olomide. 

Huku akizungumzia uhusiano kati yake na Zari Hassan msanii huyo alisema kwamba  hana uhusiano wowote wa kimapenzi na Zari ambaye ni mama wa watoto wake.

 
 

Wawili hao wamebarikiwa na watoto wawili, huku Diamond akisema kwamba kile tu wanafanya pamoja ni kusaidiana kuwalea wanao.

"Kati ya watu au wazazi wenzangu ambao naweza wasifia, yule namsifia jinsi ya kuishi kama wazazi ni Zari Hassan." Alisema Diamond.

Pia alisema kwamba alifurahi sana kuona watoto wake na ambao wana mama kama Zari walikuwa na bahati sana huku cha mno ni kumshukuru Mungu.

(Mhariri:  Davis Ojiambo)

Huku akizungumzia wanawe kukuzwa na baba mwingine alisema kwamba hana shida yeyote bora tu ana ruhusa ya kukutana na wao na kuwaona.

Watoto wake walipokuwa Tanzania wiki chache zilizopita alikuwa na fursa ya kurekodi na kutoa kibao kipya akimshirikisha mwanawe Tiffah.

Diamond alisema kwamba hawayuko pamoja na Zari na kwamba hajapata mtu au penzi wake.