Kuna msanii wa nyimbo za injili aliniitisha elfu 300 ili tufanye collabo-Mejja

Muhtasari
  • Mejja afichua haya kuhusu msanii mmoja wa nyimbo za injili
  • Mejja alidai kwamba msanii huyo alimuitisha elfu 300,00 ili akubali kufanya collabo naye
Mejja na Massawe Japanni studioni
Mejja na Massawe Japanni studioni

Staa wa nyimbo za Gengetone Mejja, akiwa kwenye mahojiano alifichua kwamba kuna msanii wa nyimbo za injili ambaye  alimuitisha elfu 300 ili akubali collabo yake.

Mejja alisema kwamba msanii huyo anafahamika sana nchini kenya.

"Nakumbuka kuna wakati tasnia ya burudani ya nyimbo za injili ilikuwa juu na imevuma sana, nilikuwa nataka kuimba kibao cha injili ili kumtukuza Mungu

 

Nilimuendea huyu msanii wa nyimbo ainjili aliniitisha elfu 150,000 za kujitolea na 150,000za kurekodi na mambo mengine

Sitaki kumtaja kwa maana sijui yuko kiwango kipi katika maisha yake," Alisema Mejja.

Alikataa kabisa kufichua jina lake bali alisem alikuwa anaimba na msanii Daddy Owen siku hizo, huku akisema kwamba sio msanii Bahati.

"Sio Bahati, kwa maana tumetoa kibao cha 'wanani' pamoja, lakni najua ni msanii ambaye alikuwa anaimba na Daddy Owen nyakati hizo

Nilishtuka sana kwa maana nilifikiria ni rafiki yangu, niliapa bele ya Mungu akiniinua hata mimi nitawainua wasanii chipukizi,"

Mejja amekuwa akifanya collabo moja baada ya nyingine huku vibao cyake vikitamba sana na kupendwa na mashabiki wake.