Mtu wa Ugali

Wakenya wamsherehekea 'Ugali man'

Charles Odongo amepongezwa na Wakenya wengi mitandaoni baada yake kupata kazi ya kufanya tangazo na kampuni ya kamari

Muhtasari

โ€ขOdongo alisisimua mitandao wiki mbili zilizopita baada ya video yake akila ugali na shauku kubwa alihusishwa kwenye tangazo lililochapishwa na kampuni ya Odibets siku ya Jumatatu.

Charles Odongo akila ugali kwa shauku kubwa
Charles Odongo akila ugali kwa shauku kubwa
Image: Twitter

Mkufunzi wa mazoezi kwa jina Charles Odongo amesherehekewa na Wakenya wengi mitandaoni baada yake kupata kazi ya kufanya tangazo na kampuni ya kamari ya Odibets.

Odongo ambaye alisisimua mitandao wiki mbili zilizopita baada ya video yake akila ugali na shauku kubwa alihusishwa kwenye tangazo lililochapishwa na kampuni ya Odibets siku ya Jumatatu.

Video from Charles Odongo

Wakenya wengi wameendelea kumpongeza Odongo ambaye kwa sasa ni mkufunzi wa mazoezi pande za Rongai huku wakimbatiza jina Ugali man.(mtu wa ugali)

Twitter trends
Twitter trends
Image: Hisani

Tazama hapa jumbe za Wakenya kwenye mtandao wa Twitter chini ya alama ya reli #UgaliMan

Tazama jumbe zingine za Wakenya wakimpongeza Odongo almaarufu kama Ugali Man  chini ya  alama ya reli #UgaliMan ( https://twitter.com/hashtag/UgaliMan?s=09 ) kwenye mtandao wa Twitter.