Akothee akashifu wanawake wanaorekodi uchi wa wenzao

Hisia hizi zinakuja siku chache tu baada ya video inayoonyesha mwanasoshalaiti Bridgit Achieng akivaa kuenezwa mitandaoni

Muhtasari

•Akothee amesema kuwa haamini mwanamke yeyote aliyeshika simu mkononi karibu naye

•.Kwenye video hiyo ambayo inaaminika kusambazwa na  mmoja wa marafiki zake, Achien'g  anaonyeshwa akivaa nguo  akiwa miongoni mwa wanawake wanaosikika nyuma ya kamera.

AKOTHEE
AKOTHEE
Image: Instagram

Mwanamuziki Esther Akoth almaarufu kama Akothee  amewasuta wanawake wanaorekodi uchi wa wanawake wenzao wakati wanavaa manguo.

Kupitia mtandao wa Instagram, mwanamuziki huyo amelaani vikali kitendo hicho huku akisema kuwa  haamini mwanamke yeyote ambaye ana simu karibu naye.

“Nimehuzunishwa sana na vitendo wanawake wanafanyia wanawake wenzao. Simuamini mwanamke yeyote aliyeshika simu mkononi karibu nami. Mbona mwanamke arekodi mwanamke mwenzake wakati anavaa? Nia yako ni ipi?” Akothee alisema

Ameeleza kusikitishwa kwake na wanawake wanaopiga wenzao picha ovyo ovyo bila kupea mtu ilani.

Wiki iliyopita nilikuwa na rafiki yangu chumbani na ghafla tochi ya kamera yake ikawaka, alijifanya kuwa anaandika kitu kwa simu. Wanawake! Wanawake!” aliandika Akothee.

Hisia hizi zinakuja siku chache tu baada ya video inayoonyesha mwanasoshalaiti Bridgit Achieng akivaa  kuenezwa mitandaoni.

.Kwenye video hiyo ambayo inaaminika kusambazwa na  mmoja wa marafiki zake, Achien'g  anaonyeshwa akivaa nguo  akiwa miongoni mwa wanawake wanaosikika nyuma ya kamera.

Achien'g ameeleza kuwa mwanamke kwa jina Linda alimualika kwake siku mbili ila wakawa na mzozo uliohusiana na pesa. Wakati alitaka kuenda aliingia bafu kuoga na mwanamke yule akarekodi video wakati alikuwa anavaa baada ya kutoka kwenye bafu.