'Wacha kulia lia,uza mandazi,'Msanii Willy Paul amwambia muigizaji Omosh

Muhtasari
  • Msanii Willy Pual kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amempa aliyekuwa muigizaji wa Tahidi High ushauri siku chache baada ya kushambuliwa na wakenya
  • Omosh alipokea kejeli kutoka kwa wakenya baada ya kutaka usaidizi mwingine kutoka kwa wakenya
Willy Paul
Willy Paul

Msanii Willy Pual kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amempa aliyekuwa muigizaji wa Tahidi High ushauri siku chache baada ya kushambuliwa na wakenya.

Omosh alipokea kejeli kutoka kwa wakenya baada ya kutaka usaidizi mwingine kutoka kwa wakenya.

Kulingana na Willy, Omosh anapaswa kuanza kazi ya kuuza mandazi ama kuenda kufanya kazi ya mjengo badala ya kuwalilia wakenya kwa mara ya pili.

"Wakenya walikusaidia, na kisha ukawageuka na kusema kuwa pesa haikufika milioni moja, hizo pesa zilikuwa za wakenya

Wacha kulia lia toka nje tafuta kazi ya mjrngo,uza mandazi ama maji, uza hizo vitu na uwacha kulia lia wakenya wanamjua mtu wa kulia

Itabidi upambane, wakenya walikusaidia mahali waliweza sisi site ni wanaume au uambie serikali ikupe kazi," Paul Alizungumza.

Omosh akiwa  kwenye mahojiano na Hiram Maina, Omosh aliwaomba Wakenya msamaha kufuatia video ambayo inaenea mitandaoni ambayo inamuonyesha akiomba pesa tena.

"Kama msanii, unaweza kutoa taarifa tu na watu huchukulia kwa uzito. "ilikuwa jambo kidogo lakini Wakenya walinisaidia sana, walinisadida wakati wangu mgumu

Tafadhali naomba msamaha niliwaumiza. Na asanteni kwa kunisamehe. Sikujua wala kufikiria Wakenya wangekasirika.

Ninajisikia vibaya sana juu ya kile kilichotokea. Samahani na hamtawahi kusikia chochote kibaya kutoka kwangu, kitu pekee mtakachosikia kutoka kwangu ni burudani," Omosh aliongea.