'Sijaachwa nimeolewa,'Nyota ndogo amjibu shabiki aliyetaka awe mke mwenza wake

Muhtasari
  • Nyota ndogo amjibu shabiki aliyetaka awe mke mwenza wake
83532576_627204834703118_8454513908795708531_n
83532576_627204834703118_8454513908795708531_n

Msanii kutoka mkoa wa pwani Nyota Ndogo, alivuma sana mwezi jana baada ya kuachwa na mumewe.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Nyota Ndogo amepakia ujumbe ambao alitumia na shabiki ambaye anatafuta mke mwenza.

Kulingana na uju be huo shabiki huyo, anatafuta mke mwenza kwani mumewe alimwambia kwamba atamletea mke mwenza.

Alimtaka Nyota Ndogo awe mke mwenza wake,ilhali msanii huyo alikataa na kuweka wazi bado ameolewa na hajaachwa na mumewe.

"Nimeolewa na ni Mama Watoto wawili. Nampenda sana Mume wangu na nitakua Muongo nikisema hanitimizii haja zangu kama Mke wake

Naishi vizuri, Watoto wangu wanasoma shule nzuri. Ila juzi kuna Wifi yangu kaniibia Siri kwamba Mume wangu ana mpango wakuongeza Mke wa Pili..

Lengo la kukuandikia waraka huu ni kukwambia kwamba mimi ni shabiki wako mkubwa tangu kitambo na nimekua nikikufuatilia kwa mda mrefu hadi niliona kwamba uliwachana na mumeo Mzungu so Ningependekeza Mume wangu akija kuniambia kuhusu swala la kuoa mke wa pili basi nikupendekeze wewe uolewe na Mume wangu tuishi pamoja na tumpende Mume wetu. Niliona una Mapenzi ya dhati na naamini utampenda Mume wetu na isitoshe Roho yako safi sana...Naomba nijibu hili Ombi langu maana mda wowote Mume wangu huenda akaja kuniambia kuhusu hili swala,"

Na Samahani endapo utahisi nimekukosea Heshima."Ujumbe wa shabiki ulisoma.

Nyota aliweka wazi kwamba hawezi kuwa mke wa pili kwa vyovyote vile.