"Kuzaa sio kunya" Nyota Ndogo awashauri wanawake kupata watoto

Nyota Ndogo amewashauri wanawake kuwa watoto ni akiba nzuri ya maisha ya usoni kwani watakuja kuwasaidia uzeeni.

Muhtasari

•Kulingana na msanii huyo kutoka Pwani, hali ya kuitwa mama ni muhimu sana katika maisha ya mwanamke.

•Amesema kuwa  sio sharti mwanamke awe kwenye ndoa ili apate watoto. Amewataka wanawake ambao hawajafunga ndoa kutoogopa kusemwa na jamii kwa kupata mtoto licha ya kutooleka.

Nyota Ndogo
Nyota Ndogo
Image: Instagram

Mwanamuziki Nyota ndogo ameshauri wanawake  kupata watoto bila kujali kama wameolewa ama hawako kwenye ndoa.

Kulingana na msanii huyo kutoka Pwani, hali ya kuitwa mama ni muhimu sana katika maisha ya mwanamke.

Kupitia mtandao wa Instagram, Nyota Ndogo amewashauri wanawake kuwa watoto ni akiba nzuri ya maisha ya usoni kwani watakuja kuwasaidia uzeeni.

Amesema kuwa  sio sharti mwanamke awe kwenye ndoa ili apate watoto. Amewataka wanawake ambao hawajafunga ndoa kutoogopa kusemwa na jamii kwa kupata mtoto licha ya kutoolewa.

"Wanawake sio wote walioandikiwa kuolewa lakini usiseme kama sitaolewa mimi sitazaa kwa kuogopa jamii itanisema nimezaa mwana haramu kwani kwa Mungu sote ni sawa. Hiyo jamii unayoiogopa ukiwa mtu mzima ndio itakayo kusema kuwa usiwatume wana wetu kwanini hukuzaa wako" Nyota Ndogo aliwaambia wanawake.

Msanii huyo ambaye ameanza kufufua taaluma yake ya uanamuziki hivi majuzi amesema kuwa amewaona wanawake wazima ambao wananyanyaswa na jamii na hata  familia zao kwa kuwa walikosa kupata watoto kwani hawakuolewa.

"Jamani, waweza kuambiwa kitu na mtu wa familia yako ikakuchoma ukatamani ardhi ipasuke ufilie mbali. Mimi naona pata watoto hata wawili huku nje"  Nyota Ndogo alisema.

Soma hapa ujumbe wake;

Nyota Ndogo ana watoto wawili, binti mmoja na mvulana mmoja na aliyekuwa mpenzi wake  wa hapo awali ambaye walitengana zaidi ya miaka kumi iliyopita. 

Kwa sasa yumo kwenye uhusiano na mzungu  Henning Nielsen kutoka Uholanzi, ingawa hawajapata watoto pamoja.

Mwezi mmoja uliopita, Nyota Ndogo alisimua wanaitandao kwa jumbe nyingi za mapenzi alizoandikia mumewe amrudie baada ya kudai kuwa alikuwa amemuacha mwezi Aprili.

Hata hivyo, alitangaza kuwa hali ya mawasiliano kati yao ilirejea  hajaonekana tena kuzungumzia swala hilo.