HONGERA DIAMOND NA ZARI

Diamond na Zari kushirikishwa kwenye kipindi cha maisha halisi cha Netflix

Wawili hao ambao wana watoto wawili pamoja ni miongoni mwa watu mashuhuri barani Afrika ambao watakuwa kwenye kipindi 'Young, Famous & African'

Muhtasari

• Diamond atakuwa raia wa pili wa Tanzania kushirikishwa kwenye Netflix baada ya mwigizaji Idris Sultan aliyeshirikishwa kwenye filamu ya "Slay' mapema mwakani.

•Diamond na Zari walichapisha jumbe kwenye kurasa zao za Instagram kuwafahamisha mashabiki wao kuhusu kipindi hicho.

Diamond na Zari
Diamond na Zari
Image: Instagram

Diamond Platnumz na aliyekuwa mpenzi wake, Zari  Hassan watashirikishwa kwenye kipindi cha Maisha Halisi cha kampuni ya Netflix.

Wawili hao ambao wana watoto wawili pamoja ni miongoni mwa watu mashuhuri barani Afrika ambao watakuwa kwenye kipindi 'Young, Famous & African' (Mwenye umri mdogo, Mashuhuri na Mwafrika) ambacho kinatarajiwa kuanza hivi karibuni.

Diamond atakuwa raia wa pili wa Tanzania kushirikishwa kwenye Netflix baada ya mwigizaji Idris Sultan aliyeshirikishwa kwenye filamu ya "Slay' mapema mwakani.

Netflix South Africa ilikuwa imepakia sura fiche kwenye mtandao wa Instagram na kuwataka mashabiki kubashiri ni kina nani hao watashirikishwa kwenye kipindi hicho

"Ni wenye umri mdogo, hawaombi msamaha kwa kuwa Waafrika, na wanakuja kwenye runinga zenu! Je waweza bashiri nyota hawa na misemo waipendao?" Netflix South Africa iliandika.

Diamond na Zari walichapisha jumbe kwenye kurasa zao za Instagram kuwafahamisha mashabiki wao kuhusu kipindi hicho.

"Kutoka Tandale hadi ulimwenguni.. Unapelekwa nyuma ya tukio ufahamu ambayo yanamgharimu nyota wa Afrika kuenea duniani na Netflix South Africna pamoja na Netflix Naija on Netflix ambacho ni kipindi cha kwanza cha maisha halisi kinachomshirikisha Simba" Diamond aliandika.

Zari naye aliagiza masshabiki wake kutazama kipindi hicho.

Mashabiki wao wameendelea kuwapongeza kufuatia tangazo hilo.