'Hayakuwa mapenzi yangu' Bahati aomba Yvette na bintiye msamaha kwa kuwaficha hapo awali

Bahati amesema kuwa kuhukumiwa sana na Wakenya kulimfanya kugeuka kuwa mnafiki na kutojivunia damu yake.

Muhtasari

•Kupitia ujumbe ambao mwanamuziki huyo aliandika kwenye mtandao wa Instagram, kuzaliwa kwa bintiye ulikuwa wakati wa furaha ila mgumu sana kwake.

•Mwanamuziki huyo ambaye kwa sasa ni mume wa Diana Marua alisema kuwa hayakuwa mapenzi yake kujifanya na kuwaficha wawili hao kutoka kwa umma ila taaluma yake ya injili ilimsukuma kufanya hivo.

Image: INSTAGRAM

Mwanamuziki Kevin Bahati amemuomba aliyekuwa mpenzi wake Yvette Obura na bintiye Mueni Bahati msamaha kwa kuwaficha kwa miaka miwili.

Bahati amesema kuwa kuhukumiwa sana na Wakenya kulimfanya kugeuka kuwa mnafiki na kutojivunia damu yake.

Kupitia ujumbe ambao mwanamuziki huyo aliandika kwenye mtandao wa Instagram, kuzaliwa kwa bintiye ulikuwa wakati wa furaha ila mgumu sana kwake.

"Ulikuwa wakati nafika kileleni kama msanii wa nyimbo za injili, punde baada ya kupata tuzo la Groove la msanii bora wa kiume na tuzo la AFRIMMA. Wakati huo nilikuwa nahukumiwa sana, najua mnanielewa. Niliishia kuwa mnafiki badala ya kujivunia damu yangu" Bahati aliandika.

Mwanamuziki huyo ambaye kwa sasa ni mume wa Diana Marua alisema kuwa hayakuwa mapenzi yake kujifanya na kuwaficha wawili hao kutoka kwa umma ila taaluma yake ya injili ilimsukuma kufanya hivo.

"Hayo hayakuwa mapenzi yangu ila kwa kile nilichokuwa nafanya , muziki wa injili. Haikufaa kuwa hivo, si vyema kuwa mnafiki." Bahati aliendelea kusema.

Hata hivyo, alimshukuru bintiye kwa kuja maishani mwake na Yvette kwa kuchagua amani badala ya fujo na kuwezesha ulezi wa bintiyao kuwa rahisi.

Bahati pia alimwandikia Yvette kuwa angependa kualikwa kwenye harusi yake kwani alikuwa amesoma kwenye blogu kuwa alipata mchumba mzuri.

"Pia nilisoma kwenye blogs kuwa umepata mtu handsome. Tafadhali ningefurahia kualikwa kwenye harusi yako. Mungu abariki maisha yako, safari na yote unayoyafanya" Bahati alimwandikia Yvette.