Hongera! Mcheshi YY asisimua wanamitandao baada ya kumjengea mamaye nyumba

Akothee alisema kuwa kuwa kunao watu wengi ambao wanaendesha magari makubwa ila hawajui wanakolala wazazi wao au wanachokula.

Muhtasari

•Msanii huyo alipakia picha mbili ya kwanza akionyesha hali duni ambayo mamake alikuwa akiishi katika kisha ya pili ikionyesha nyumba maridadi aliyomjengea mamake.

•Ujumbe wa kipekee wa msanii huyo ulikuwa "Nakupenda mama yangu ❤️❤️❤️  "

Image: INSTAGRAM//YY COMEDIAN

Mcheshi Oliver Otieno almaarufu kama YY anajivunia kukamilisha ujenzi wa nyumba ya mama yake.

YY ambaye alipata umaarufu mkubwa kutokana na kipindi cha Churchill Show alitangaza mafanikio hayo kwenye ukurasa wa Instagram.

Msanii huyo alipakia picha mbili ya kwanza akionyesha hali duni ambayo mamake alikuwa akiishi katika kisha ya pili ikionyesha nyumba maridadi aliyomjengea mamake.

Tofauti na wasanii wengine ambao hupendelea kuambatanisha tangazo la mafanikio  kama hayo na jumbe refu, YY hakuwa na maneno mengi ya kuwaambia mashabiki ila tu kumwambia mamaye jinsi anavyompenda.

Ujumbe wa kipekee wa msanii huyo ulikuwa "Nakupenda mama yangu ❤️❤️❤️  "

Wanamitandao wengi ikiwemo watu mashuhuri walijumuika kumpongeza YY kwa hatua hiyo. Kati ya waliompongeza ni pamoja na Jalang'o, Ringtone, Akothee, Owago, Kabi wa Jesus, Mulamwah, Butita, Billy Miya kati ya wengine wengi.

Hizi hapa baadhi ya jumbe:

@djshiti_comedian👏👏👏👏👏👏👏👏👏@mulamwahCongrats papa 👏🙌

@itsakukudangerPolo mor baa

@jackyvike👏🏾👏🏾👏🏾@djmokenyaGood one - one good way to tap blessings

@guardianangelglobalBROOOOO 👊👊👊👊👊🙏🙏🙏🙏

@jabidii_musicCongratulations 👏👏🙏

@billymiya🔥🔥🔥 Polo Mor!

@Jalangoo Mungu wewe!! Bro may you never lack!

@EddiebutitaMungu akuzidishie👏👏👏👏

Akothee alisema kuwa kitendo cha wasanii kuwatuza wazazi wao ni nadra sana.  Alisema kuwa kuwa kunao watu wengi ambao wanaendesha magari makubwa ila hawajui wanakolala wazazi wao au wanachokula.

"Hata Mungu aliko nina hakika amesimama. YY una miaka mingapi? Wanaume wa rika lako wanafurahia maisha jijini. Ja SDA mbona usitumie pesa zako Dubai??" Akothee alimtania YY.

"Ni  hatua iliyowazwa aje, zawadi la mwana kwa mamaye. Wanaume wanaendesha magari makubwa jijini bila taarifa wazazi wao wanalala wai au wanakula nini. Omera YY Comedian umecheza kama mwanaume" Aliendelea kusema.