Kupigwa na mume mara moja moja ni afya- Aliyekuwa mpenzi wa Diamond, Wema Sepetu adai

Amesema kuwa tendo la mwanaume kupiga mkewe mara moja moja ni afya.

Muhtasari

•Hata hivyo,Wema Sepetu amesema kuwa yafaa mwanaume ampige mkewe kidogo tu mara moja moja baada ya kukawia wala sio kila siku.

•Mwigizaji huyo amesimulia kisa kimoja ambapo mpenzi wake wa zamani aliwahi kumpiga licha ya kuwa alikuwa ameapa hatawahi kumpiga mwanamke yeyote. Hata hivyo amesema kuwa alifurahia kitendo hicho.

Image: INSTAGRAM// WEMA SEPETU

Mwigazaji mashuhuri toka Bongo Wema Sepetu ameacha wanamitandao wengi midomo wazi baada ya kukiri huwa anapendelea mpenzi wake akimpiga mara moja moja.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, msanii  huyo ambaye aliwahi kuwa mpenzi wa staa wa Bongo Diamond Platnumz amesema kuwa tendo la mwanaume kupiga mkewe mara moja moja ni afya.

Hata hivyo,Wema Sepetu amesema kuwa yafaa mwanaume ampige mkewe kidogo tu mara moja moja baada ya kukawia wala sio kila siku.

"Kupigwa na baby wako kuna raha yake, haswa pale kwenye  kubembelezana. ila sasa sio tupigane kama wezi.. Kidogo tu sio mbaya.. Alafu iwe mara moja sio kila siku..

Sio lazima tufanane, kuna wasio penda kupigwa ila kwangu kushtua shtua mara moja moja ni afya jamani" Sepetu aliandika.

Mwigizaji huyo amesimulia kisa kimoja ambapo mpenzi wake wa zamani aliwahi kumpiga licha ya kuwa alikuwa ameapa hatawahi kumpiga mwanamke yeyote. Hata hivyo amesema kuwa alifurahia kitendo hicho.

"Nakumbuka zamani wakati naanza mapenzi na mwanaume fulani alishanitamkia hajawahi na hatowahi kumpiga mwanamke.. Ila kwangu bwaba akagonga mwamba na hicho kiapo. Kiukweli nilienjoy  sana" Alisema Wema Sepetu.

Mwaka wa 2011, nyota huyo wa uigizaji alimshtaki aliyekuwa mpenzi wake Diamond Platnmuz kwa madai ya kumdhulumu kimwili. Hata hivyo Diamond hajawahi kuzungumzia suala hilo.