Mwanawe naibu rais William Ruto azungumzia madai kuwa yeye ni shoga

Muhtasari

•Kwenye video hiyo ambayo ilirekodiwa katika hafla ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa,  Nick anaonekana akiwekwa mkufu wa dhahabu na jamaa mwenye asili ya kihindi huku wengine waliokuwa wamehudhuria wakishangilia.

•Wakili huyo ameeleza kwamba kupokea zawadi kutoka kwa rafiki wa jinsia sawa hakumaanishi kuwa lazima kuna uhusiano wa kimapenzi kati yao.

Image: FACEBOOK// NICK RUTO

Nick Ruto, mwanawe naibu rais William Ruto amekuwa akizungumziwa sana mitandaoni baada ya video inayoonyesha akiwekwa mkufu shingoni na mwenzake wa kusambazwa mitandaoni.

Kwenye video hiyo ambayo ilirekodiwa katika hafla ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa,  Nick anaonekana akiwekwa mkufu wa dhahabu na jamaa mwenye asili ya kihindi huku wengine waliokuwa wamehudhuria wakishangilia.

Baada ya video hiyo kusambazwa mitandaoni baadhi ya  wanamitandao walimshutumu mwana huyo mkubwa wa naibu rais kuwa shoga.

Kufuatia madai hayo, Nick Ruto alitumia ukurasa wake wa Facebook kujibu huku akiwaagiza watu kuelewa thamani ya urafiki.

Wakili huyo ameeleza kwamba kupokea zawadi kutoka kwa rafiki wa jinsia sawa hakumaanishi kuwa lazima kuna uhusiano wa kimapenzi kati yao.

"Tengenezeni uhusiano wenu na msherehekeane. Kama unaweza, watuze marafiki wako kama unavyoweza wakati wa hafla muhimu kama siku ya kuadhimisha kuzaliwa, maadhimisho ya miaka, harusi n.k.

Hii itasaidia kuelewa thamani ya urafiki na kufahamu kuwa kutuza rafiki wa jinsia sawa ama tofauti  hakumaanishi kuwa kuna uhusiano wa kimapenzi kati yao. Nawashukuru kwa jumbe zenu za kuadhimisha siku ya kuzaliwa na zawadi zenu" Nick Ruto aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Nick ambaye pia ni mfanyibiashara alisherehekea kufikisha miaka 30.