"Ningekuoa tena na tena" Gavana Kibwana aandikia mkewe ujumbe maalum wanapoadhimisha miaka 43 ya ndoa

Muhtasari

• Kibwana amefichua kwamba alijitosa kwenye ndoa akiwa na umri wa miaka 24 tu.

Image: TWITTER// KIVUTHA KIBWANA

Gavana Kivutha Kibwana pamoja na mkewe Nazi Kibwana wanaadhimisha miaka 43 ya ndoa yao.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Kibwana amesema kwamba alijitosa kwa ndoa akiwa na umri wa miaka 24 tu.

Kibwana amesema kwamba ndoa yake haijakuwa laini kila wakati, imekabiliwa na panda shuka ila pamekuwa na upendo mkubwa kati yao.

"Tunasherehekea miaka 43 ya ndoa leo. Nilioa nikiwa na miaka 24. Tumekuwa na upendo wa Mungu kila wakati. Kumekuwa naupendo na  panda shuka. Kama Simi alivyoimba, mapenzi hayajali, unachagua utakayependa na unawapenda hadi mwisho. Ningekuoa tena na tena. Maadhimisho mazuri ya miaka" Kibwana aliandika.

Wanandoa hao walifunga pingu za maisha mwaka wa 1978. Licha ya gavana Kibwana kuwa kwenye siasa kwa muda mrefu, sio mengi yanajulikana kuhusu Bi Nazi Kibwana kwani anapendelea kuishi maisha ya kisiri