'Poleni kwa kuwafanya mjisikie vibaya,'Akothee aapa kuweka uhusiano wake kwenye faragha

Muhtasari
  • Msanii na mjasirimali Akothee hatashiriki tena maelezo ya uhusiano wake kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii
Nelly Oaks na Akothee
Nelly Oaks na Akothee
Image: INSTAGRAM//NELLY OAKS

Msanii na mjasirimali Akothee hatashiriki tena maelezo ya uhusiano wake kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Kulingana na Akothee, amefikia uamuzi huo baada yakupokea simu kutoka kwa 'single mothers' kuweka maisha yake ya mapenzi kibinafsi au kwenye faragha.

"Single mothers wameniuliza nisiweke maisha yangu ya mapenzi kwenye mitandao ya kijamii hadi wote tutakapopata wanaume, nimewasikia lakini nitajuaje kuwa nyinyi mko tayari?" Akothee aliandika.

Pia msanii huyo aliwashauri akina mama hao wanawake wasipinge kuwa na wenzi wa kiume.

Aliwaambia wawe wazi kujaribu uhusiano kadhaa hadi watakapompata mwanamume ambaye yuko tayari kuwa nao kwenye uhusiano wa kimapenzi.

"Samahani kwa kukufanya ujisikie vibaya lakini kumbuka kila mwanamke anahitaji mwanaume ili kudhibiti akili zake za kawaida, Mungu hakuwa mjinga kumwuliza Noah ajenge safina ambayo ingeweza kuchukua watu 2,2,2 Wewe ni nani kupigana na mwili

Vitu vingine haviwezi kubadilishwa, ikiwa uhusiano huu haufanyi kazi, endelea kujaribu mpaka uupate sawa Mambo yenu ya mimi sihitaji mwanaume Iliisha na corona, corona alitudhalilisha wengi wetu. "

Kuanzia leo, Akothee atashiriki tu habari za uchumba, harusi, au ujauzito.

"Niambie wakati nyinyi nyote mna mtu. Nitarudi Kuanzia leo nitatuma tu 1 1. Uchumba wangu 2. Harusi yangu 3. ujauzito wangu. Zilizobaki hii ni kubwa Je, naenda? Mambo ya wanandoa malengo wachia hapo, " alisema.