"Hii safari ni ngumu, aulize Baha!" Willy Paul, Mulamwah na wanamitandao watoa maoni baada ya Diana Marua kujitosa muzikini

Muhtasari

•Siku moja baadae malkia huyo mwenye umri wa miaka 32 alitoa kibao chake cha kwanza  'Hatutaachana' ambacho cha kushangaza zaidi kiliweza kupata zaidi ya watazamaji laki tatu ndani ya masaa 12.

•Mwanamuziki Willy Paul alipoulizwa maoni yake kuhusiana na hatua ya Diana kuingia kwenye muziki  kwanza aliangua kicheko kikubwa kabla ya kumshauri atie bidii na aombe Mungu ili afanikiwe.

•Mtumizi mmoja wa Twitter anayejitambulisha kama @OnlyWangui alisema huenda Diana ni zile mawe ambazo Bibilia inasema zitaimba watu wakikataa kumuimbia Mungu.

Image: INSTAGRAM// DIANA MARUA

Siku ya Jumamosi mke wa mwanamuziki Bahati, Diana Marua alizindua taaluma yake ya muziki akijitambulisha kama rapa Diana B.

Diana B alizinduliwa kama mwanamuziki katika hafla iliyohudhuriwa na watu kadhaa ikiwemo wasanii na watu mashuhuri.

Siku moja baadae malkia huyo mwenye umri wa miaka 32 alitoa kibao chake cha kwanza  'Hatutaachana' ambacho cha kushangaza zaidi kiliweza kupata zaidi ya watazamaji laki tatu ndani ya masaa 12.

Wakenya wameendelea kutoa hisia na maoni mbalimbali kuhusiana na kuingia kwa Diana Marua kwenye muziki.

Mwanamuziki Willy Paul alipoulizwa maoni yake kuhusiana na hatua ya Diana kuingia kwenye muziki  kwanza aliangua kicheko kikubwa kabla ya kumshauri atie bidii na aombe Mungu ili afanikiwe.

"Diana naweza mwambia hii safari ni ngumu, aulize Bahati. Ni ngumu lakini akitilia maanani, bidii na aombe Mungu atamsikia" Willy Paul alimshauri Bahati.

Mchekeshaji David Oyando almaarufu kama Mulamwah akiwa kwenye mahojiano na Mungai Eve vilevile kwanza alicheka baada ya kuulizwa maoni yake kuhusiana na hatua ya Diana B kabla ya kumshauri aendelee na muziki wake.

"Hiyo rap inaweza, kwanza ameingia na madiss mbaya  sana. Ameingilia mpaka Rihanna, beef zake hata si za Kenya. Hata hivyo, ni poa bora tu anapiga kazi legit. Hii Kenya ni kuhustle bana, watu wako biashara. Ikikataa huku unarap. Ikikataa unafungua butchery unauza nyama" Mulamwah alisema.

Mamia  ya Wakenya walioa maoni mbalimbali mitandaoni wengine wakimpongeza Diana huku wengine wakimkosoa.

Mtumizi mmoja wa Twitter anayejitambulisha kama @OnlyWangui alisema huenda Diana ni zile mawe ambazo Bibilia inasema zitaimba watu wakikataa kumuimbia Mungu.

@loe_loise Ni kama uliimba ki BAHATI mbaya

@kisav_u Wimbo ni mzuri sana, shida ni ati dee alizindua na nguo mbaya

@fideris.mwende Diana umeshinda artist wengi, hongera Dee wetu. na bado umeanza, go go go gal

@charitymichael@ Yaaas!! Ongeza volume... hii ni nzuri