"Nakushukuru sana, nakupenda sana!" Baby mama wa Bahati, Yvette amlimbikizia Diana Marua sifa kochokocho

Muhtasari

•Yvette alimshukuru Diana kwa kujitolea kumpa binti yake malezi mazuri kila anapotembelea familia ya baba mzazi, Bahati

•Siku ya Jumatatu, binti ya Yvette na Bahati, Mueni Bahati alifikisha miaka sita.

Yvette Obura na Diana Marua
Yvette Obura na Diana Marua
Image: INSTAGRAM

Baby mama wa mwanamuziki Bahati, Yvette Obura almaarufu kama mama Mueni amemlimbikiziasifa kochokocho mpenzi wa sasa wa mwanamuziki huyo, Diana Marua kwa kuwa mama wa kambo mzuri kwa bintiye.

Alipokuwa anatoa hotuba yake katika hafla ya kumzindua Diana Marua kama mwanamuziki, Yvette alisimulia jinsi mke wa Bahati amefanikisha ulezi wa pamoja wa Mueni.

Yvette alimshukuru Diana kwa kujitolea kumpa binti yake malezi mazuri kila anapotembelea familia ya baba mzazi, Bahati

"Ningependa kukushukuru kwa moyo wote kama mama . Umeifanya rahisi sana kwangu. Baada ya kila kitu ambacho tumepitia, huwa namwomba Mungu jambo moja, mtu ambaye atamlea mtoto wangu upandehuu, aifanye na moyo wake wote. Na umefanya na kila kitu ulicho nacho" Mama Mueni alisema.

Yvette alifichua kuwa binti yake huwa anatamani sana kurudi kwa kina Diana kila anapotoka kuwatembelea.

"Mnajua watoto huwa hawadanganyi. Kila anaporudi nyumbani baada ya kuwatembelea, kila wikendi huwa ananiambia eti anataka kurudi kwa babake. Ata tulikosana na Mueni sana kwa sababu anataka kuja kwenu kabisa kabisa. Ni miujiza, ni baraka ni jambo la ajabu.. leo, nakushukuru sana na nakupenda sana mbele ya kila mtu" Yvette alisema.

Siku ya Jumatatu, binti ya Yvette na Bahati, Mueni Bahati alifikisha miaka sita. Wawili hao wamekuwa wakishirikiana katika ulezi wa mtoto wao licha ya kutengana miaka kadhaa iliyopita.