Staa wa Bongo Ben Pol atowa wimbo Mpya kuhusu mazingira

Muhtasari

•Staa wa Bongo Ben Pol , maarufu kwa kibao chake 'Moyo Mashine'  atakuwa nchini Kenya kuanzia tarehe 27 Juni hadi 3 Julai.

 


Ben Pol
Image: Instagram

Staa wa Bongo Ben Pol , maarufu kwa kibao chake 'Moyo Mashine'  atakuwa nchini Kenya kuanzia tarehe 27 Juni hadi 3 Julai.

Akiwa katika ziara hiyo, atazindua  wimbo mpya wa 'Kijanisha' ambao ameshirikisha wanamuziki wengine Christina Shusho, joh Mkini Frida Amani, Justdigit na Wakfu wa Lead ili kuhamashisha jamii kuchukua hatua kurejeshi Miti duniani.

Kijanisha maana yake ni regreen the earth (kurejesha rangi ya kijani kibichi duniani) , wimbo huo unaleta ujumbe na ahadi ya harakati ya kuweka kijani kibichi moja kwa moja kwenye mawimbi ya Tanzania na kwingineko.

Mabadiliko ya hewa yanathiri kila kiumbe na niwajibu wa kila mmoja kuchukua hatua kupunguza hadhari zake, wasanii hao wanasema kupitia mawasiliano watahamashisha kila mmoja mbinu asili za kutunza Mazingira.

Baada ya kujionea athari za mabadiliko ya hali ya hewa  na uharibifu wa ardhi, Christina Shusho, Joh Makini, Frida Amani na Ben Pol watatumia sauti zao kwa pamoja kuhimiza kila mmoja kujiunga na harakati za kuimarisha upanzi wa miti 'Dig in'.

Kwa kupitia  muziki wao, wasanii hao watahamashisha umma  kuhusu mbinu kama uchimbaji visima  vya kuhifadhi maji.