'Sikupata usingizi,'Daddy Owen amuomboleza msanii Ngashville

Daddy Owen ameandika ujumbe wa hisia kwenye ukurasa wake wa instagram kufuatia kifo cha rafiki yake.

Muhtasari
  • Akishiriki nyakati ambazo wamekuwa pamoja, Daddy Owen alikumbuka kumuona Ngashville akiwa na furaha, huzuni, akihangaika, akifanikiwa maishani. Alimtaja kuwa mpiganaji

Tasnia ya burudani na muziki inaomboleza kifo cha msanii mashuhuri Ngashville.

Daddy Owen ameandika ujumbe wa hisia kwenye ukurasa wake wa instagram kufuatia kifo cha rafiki yake.

Akishiriki nyakati ambazo wamekuwa pamoja, Daddy Owen alikumbuka kumuona Ngashville akiwa na furaha, huzuni, akihangaika, akifanikiwa maishani. Alimtaja kuwa mpiganaji.

Owen alifichua kwamba alimuona Ngashville akipigana kwenye kitanda cha hospitali.

Akilini alijua kuwa madaktari watampatia Ngashville dawa tu na kurejea nyumbani Habari za kifo chake zilimfanya ajifanye ana nguvu mbele ya watu lakini alipofika nyumbani hakupata usingizi.

"NGASHVILLE.. Bro manze I have seen u happy.. sad.. struggling.. making it and all through life! Wewe ni mpiganaji! Jana niliona unapigana kwenye kitanda cha hospitali, av seen it all with u Ngash .. lakini ilikuwa ni wakati, wakati wa kuwa na BWANA, ilibidi nijifanye mbele ya kila mtu jinsi nilivyokuwa na nguvu wakati huo, lakini nilienda. nyumbani sikupata usingizi.. nilipitia video na picha zetu zote.. ilikuwa ngumu, group letu la WhatsApp la THE THREE MUSKETES with u n @duncomusic sasa halitakuwa na maana! Tulipoingia hosi juzi nilifikiri ni madawa tu utapewa then u go home.. but I guess the home I thought was totally different... U r now HOME WITH THE Lord. R.I.P Ngash, R.I.P Ngashville mapoz!.. R.I.P Mukwaru! RIP Mzuri!," Aliandika Owen.