Hata uende wapi kuongeza dawa hiyo nguvu tushaijua-Ujumbe wa Jimal wenye kutatanisha

Kupitia kwenye mitandao yake ya kijamii, alitangulia kuandika ujumbe wa siri kwa mashabiki wake alipokuwa akihutubia mtu ambaye hakusema.

Muhtasari
  • ake ilikuwa inasema hata ukienda popote kuongeza dawa sote tunajua nguvu hiyo inatoka wapi
Mfanyabiashara Jimal Rohosafi
Mfanyabiashara Jimal Rohosafi
Image: Instagram//JimalRohosafi

Mjasirimali Jimal Roho Safi kwa muda sasa amekuwa akiwapa mashabiki wake ushauri ,kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram.

Kupitia kwenye mitandao yake ya kijamii, alitangulia kuandika ujumbe wa siri na wenye maswali mengi kwa mashabiki wake alipokuwa akihutubia mtu ambaye hakusema.

Kulingana na posti yake ilikuwa inasema hata ukienda popote kuongeza dawa sote tunajua nguvu hiyo inatoka wapi kwani ushauri wake kwa mtu huyo ni kumrudia Mungu, kufanya kazi kwa bidii na kusonga mbele.

"Akili ya mtu haijawahi pumzika hata uende wapi kuongeza dawa nguvu hiyo tushaajua,ushauri wangu ni kuwa mrudie Mungu, fanya kazi kwa bidii na undelee na maisha yako,sumu,washauri wasiostahili, wakati wa Mungu karantini,"Aliandika Jimal.

Ni ujumbe uliowaacha mashabiki na wanamitandao na maswali mengi yasiyo na majibu.