Boyz II Men kutimba Kenya mara ya kwanza kwa hisani ya Radio Africa ikishirikiana na Stanbic

Stanbic Yetu Festival ni tamasha ambalo linafadhiliwa na kuwezeshwa na benki ya Stanbic kwa ushirikiano na kampuni ya Radio Africa.

Muhtasari

• Lengo la tamasha hili ni kuimarisha muziki ambao ni kiunganishi chenye nguvu ya aina yake kwa binadamu wa matabaka yote,

• Kenya litakuwa taifa la kwanza kukanyagwa na kundi la Boyz II Men mahsusi kwa Stanbic Yetu Festival kabla ya kuelekea Uganda na Afrika Kusini.

Kundi la Boyz II Men kukanyaga Kenya kwa mara ya kwanza kwa hisani ya Stanbic Yetu Festival.
Kundi la Boyz II Men kukanyaga Kenya kwa mara ya kwanza kwa hisani ya Stanbic Yetu Festival.
Image: RADIO JAMBO.

Kwa mara nyingine tena kampuni ya Radio Afrika ina furaha kutangaza kushirikiana na Stanbic Bank kukuletea burudani ya kukata na shoka ya Stanbic Yetu Festiva mnamo Jumamosi ya Juni 10 mwaka jijini Nairobi.

Kufuatia mafanikio makubwa ya tamasha kama hili la mwaka jana liliyofanyika katika ukumbi wa Carnivore na kumleta msanii mkubwa wa Soul na RnB kutoka Marekani Anthony Hamilton, aliyekaribishwa ukumbini na Otile Brown na June Gachui, mwaka huu pia Stanbic Yetu Festival kwa kushirikiana na Radio Africa watakuletea burudani babu kubwa kutoka kwa wasanii wa Kenya na wa kimataifa wanaofahamika sana kwa midundo ya Rhythm na Blues.

Tamasha la Stanbic Yetu la mwaka huu si la kukosa maana wasanii waliotamba kwa miongo mingi katika kitivo cha muziki wa RnB, BoyzII Men watakiwasha mubashara kwenye ukumbi.

Kikundi cha BoyzII Men kilifafanua upya muziki maarufu wa RnB na kinaendelea kuunda vibao vya kudumu vinavyovutia mashabiki kote na vizazi vyote.

Tuzo 4 za Grammy za kikundi hicho ni tone tu la ufuta katika bahari ya mafanikio yao. Katika taaluma yao ya miaka 25, Boyz II Men wameshinda tuzo tisa (9) za ajabu za Muziki za Marekani, Tuzo tisa (9) za Soul Train, tatu (3) Tuzo za Billboard, miongozi mwa tuzo zingine.

Kenya ni taifa la kwanza katika ziara yao ya muziki barani Afrika ambapo watakanyaga. Pia watatumbuiza nchini Uganda na Afrika Kusini.

Tamasha hilo pia litashuhudia baadhi ya Dj bora wa Kenya akiwemo DJ G-Money, DJ Forro, Dj Shaky, DJ Grauchi, CNG na DJ Dream.

Kando na Muziki, tamasha hilo pia halitakamilika pasipo na vinywaji vya kujiburudisha. Mwaka huu Pernod Ricard Kenya watakuwepo kama wafadhili rasmi kwa upande wa vinywaji.

Hoteli ya Sankara ni mshirika wa hoteli kwa mara nyingine kwa ajili ya Tamasha la Stanbic Yetu Festival huku mshirika wa usafiri angani akiwa ni Kenya Airways.

Benki ya Stanbic na Kampuni ya Radio Africa kupitia Tamasha la Stanbic Yetu linatafuta kuimarisha muziki, a kiunganishi chenye nguvu cha binadamu, ili kuleta uhai wa ahadi ya chapa ya Stanbic "INAWEZA KUWA" kwa kuunda uzoefu wa muziki wa moja kwa moja wa kupendeza na wa kusisimua nchini Kenya, unaofanya uwezekano kuwa kweli na ndoto iwezekanavyokwa mamilioni ya Wakenya.