'Umekuwa mtu bladifakin,'Mashabiki wamsuta Willy Paul baada ya haya

Muhtasari
  • Willy Paul asutwa na mashabiki baada ya kusema atawafichua wasanii hawa
Willy Paul
Willy Paul
Image: Instagram

Msanii Willy Paul ni miongoni mwa wasanii ambao wanapenda kuvuma sana kwenye mitandao ya kijamii.

Kupitia kwenye ukutasa wake wa instagram msanii huyo alidai kwamba kuna wasanii katika tasnia ya burudani ni mashoga na wasipomuomba msamaha ata wafichua.

Willy Paul alitangaza kutoa albamu yake na kama wasanii wengi wanavyotumia mtindo wa kutafuta kiki ili nyimbo zao zitazamwe endapo wamezitoa labda anatumia mtindo ho huo.

Haijabainika ni wasanii wapi Willy Paul anataka kuwafichua au anatafuta kiki tu kwa ajili ya albamu yake.

Msanii huyo aliwapa wasanii hao masaa 24, wamuombe msamaha la sivyo ata mwaga unga.

"Nawapa masaa 24 kuomba msamaha ama maji imwagike na sisemi tena. hawa wasanii wa kiume wanajijua. nipigieni simu na muombe msamaha!!Tizama hii video!!," Aliandika Willy.

Wasani hawakupendezwa na kitendo cha Willy Paul, huku asilimia kubwa ikimsuta kwa mambo ambayo amekuwa akifanya ili kutafuta kiki.

Hizi hapa baadhi ya hisia za mashabiki.

dkkwenyebeat: Sema Serikali ikutafutie Kazi

kairu_nexus: Wewe sasa umekuwa mtu bladifakin

nyala_niccur: 😂😂wacha kututishia😂

jennytania5: Khai😂😂😂 serikali ilikataa kutupea kazi kabisa

lisa_hanyofficial: Why beg Willy? Leave them alone,do your thing and let them make money anyhow!

ramsey_leziki: 😂😂😂 we tuambie ni kina nani hao😂 wacha story mingi😂

beckychris_odhis: Umeanza kua bladifakni sasa wacha hizo kiki as ringtone

Je msanii huyo anafanya hayo kwa ajili ya albamu yake au madai ake ni ya ukweli?