Sikupoteza kazi yangu kwa ajili ya Jemutai-Hamo aweka mambo wazi

Muhtasari
  • Baada ya drama kati ya mchekeshaji Hamo na Jemutai kuenea sana mitandaoni, Hamo alitoka aliacha kazi huku madai yakiwa kuwa Jemutai  ndiye alisababisha kufutwa kwake
  • Haya yalijiri baada ya Jemuta kudai kwamba Hamo hajakuwa akijikumikia mahitaji ya wanawe kwa muda sasa
Jemutai na Hamo
Jemutai na Hamo
Image: Hisani

Baada ya drama kati ya mchekeshaji Hamo na Jemutai kuenea sana mitandaoni, Hamo alitoka aliacha kazi huku madai yakiwa kuwa Jemutai  ndiye alisababisha kufutwa kwake.

Haya yalijiri baada ya Jemuta kudai kwamba Hamo hajakuwa akijikumikia mahitaji ya wanawe kwa muda sasa.

Kupitia kwenye youtube wawili hao waliyachukua maswali ya mashaiki ya kuyajibu,mmoja wa mashabiki wao aliuliza kama Jemutai ameolewa na Hamo na jibu lake lilikuwa hili;

"Kisheria sijaolewa, hatujapeleka mahari,"Jemutai alisema.

Pia Hamao alikuwa na haya ya kusema.

"Ingekuwa ni jambo nafanya peke yangu naweza enda kesho, ni furaha kudensi na mke wako lakini mipango iko,"

Pia alipata swali kuwa wanaishi vipi baada ya kusababisha kufutwa kwa Hamo.

"Sikupoteza kazi yangu kwa ajili ya Jemutai nilikuwa nimejiuzulu mwezi mmoja kabla ya drama,"

Naye Jemutai alisema kuwa;

"sikusababisha Hamo kufutwa kazi alikuwa ashaajiuzulu mwezi mmoja kabla,"