Kwa nini umpige mwanamke,'Massawe Japanni baada ya mumewe Janet Mbugua na nguguye kudaiwa kumpiga mwanamke

Muhtasari
  • Eddie Ndichu, mume wa mtangazaji wa Runinga Janet Mbugua anadaiwa kupigana kwenye hoteli ya jiji mwishoni mwa wiki
Eddie Ndichu na Paul Ndichu
Image: Hisani

Eddie Ndichu, mume wa mtangazaji wa Runinga Janet Mbugua anadaiwa kupigana kwenye hoteli ya jiji mwishoni mwa wiki.

Katika ujumbe wa moja kwa moja kwa mwanaharakati Boniface Mwangi, mwanamke alisema Eddie Ndichu na pacha wake Paul Ndichu walimshambulia yeye na dada yake.

“Jana dada yangu na mimi tulishambuliwa na mapacha wa Ndichu kwa kuwakataa kwa heshima. Walitishia kutupiga risasi na kuharibu maisha yetu

Dada yangu alinyongwa na Paul Ndichu wakati mpenzi wake aliyemjia alikuwa akinyongwa na Eddie, "ilisomeka ujumbe uliotumwa kwa Boniface Mwangi.

Katika ujumbe wake, mwathiriwa alisema tukio hilo limemwacha akiwa na hofu.

Kwenye video iliyoshirikiwa na Boniface, mtu mmoja anaonekana akiharibu gari lililokuwa limeegeshwa nje ya hoteli.

Kulingana na ripoti ya wanawake hao, wanadai wanaume wawili ni Paul Ndichu na ndugu yake Eddie Ndichu, na mwingine ni mpenzi wa dada yake.

Wakati wa kipindi cha bustani la Massawe, mtangazaji massawe amekashifu vikali  wanaume ambao wamekuwa na mazoea ya kuwapiga wanawake kila kuchao.

"Video ya mumewe Janet Mbugua, ambayo inasambaa na kuenea sana mitandaoni ni ya kusitikisha, ukitazama video hiyo ni ya kusitikisha, wanaume wamekuwa wakiwachapa wanawake kila kuchao

Kwa nini umchape mwanamke," Massawe aliuliza.