"Najihisi nimebarikiwa kupata mapenzi ya kweli mikononi mwako" Vera Sidika amsifia mumewe Brown Mauzo

Muhtasari

•Haijulikani wazi umri ambao mwanamuziki huyo alihitimu lakini Vera ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 32 aliwahi kufichua kwamba mumewe amemzidia umri kwa miaka miwili.

Image: INSTAGRAM// VERA SIDIKA

Mwanamuzuki Fredrick Mtinda almaarufu kama Brown Mauzo aliadhimisha siku yake ya kuzaliwa Ijumaa (Desemba 31, 2021).

Mwanasoshalaiti Vera Sidika alitumia ukurasa wake wa Instagram kusherehekea siku hiyo maalum kwa mumewe na kumnakilia ujumbe mtamu.

Katika ujumbe wake, Vera alimsifia Mauzo sana kama mume na baba bora zaidi duniani huku akisema anajivunia sana kuitwa mke wake.

"Heri za siku ya kuzaliwa kwa mume bora duniani @brownmauzo254 ❤️😩Ninahisi nimebarikiwa kupata upendo wa kweli mikononi mwako. Najivunia kukuita mume wangu. Ubarikiwe na yote ambayo umewahi kutamani mpenzi wangu @brownmauzo254 .NAKUPENDA! ❤️ Baba BORA kuliko wote!!!! 😩🙌 Pacha wa @princess_asiabrown 😂😂" Vera alimwandikia mumewe.

Haijulikani wazi umri ambao mwanamuziki huyo alihitimu lakini Vera ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 32 aliwahi kufichua kwamba mumewe amemzidia umri kwa miaka miwili.

Wawili hao wamekuwa kwenye mahusiano kwa kipindi cha mwaka mmoja na walibarikiwa na mtoto wa kike Asia Brown mnamo mwezi Oktoba.