Femi One aeleza Changamoto alizokumbana nazo kwenye Muziki

Muhtasari

•Femi One ameamua kufungua roho na kueleza bayana mambo ambayo wanamuziki chimpukizi hasa wa mtindo wa Sheng upitia hadi kufikia kiwango cha kutambulika na Wakenya.

•Alieleza tasnia ya muziki ijakuwa rahisi hasa kwa wanasanii ambao wanaochipuka na kuwaomba wawe na Imani kwamba kutokana na kazi zao watatambulika na kila mtu nchini .

femi one
femi one
Image: Hisani

Mwanamuziki mashururi wa mtindo wa kufoka au rap Wanjiku Kimani almaarufu Femi One ameamua kufungua roho na kueleza bayana mambo ambayo wanamuziki chipukizi hasa wa mtindo wa Sheng hupitia hadi kufikia kiwango cha kutambulika na Wakenya.

kupitia ukurusa wake wa Twitter, alieleza tasnia ya muziki haijakuwa rahisi hasa kwa wanasanii ambao wanaochipuka na kuwaomba wawe na imani kwamba kutokana na kazi zao watatambulika na kila mtu nchini .

Kulingana naye, wasanii wenye lafudhi ya Kingereza walimkataa kwa sababu alikuwa anazungumza na kurap kwa Sheng. Lakini hayo yalibandilika wakatiwalipogundua aina yake ya muziki.

"Sekta ya burudani daima imekuwa ya daraja la ASF!! Ata nyinyi wasanii wa kuimba kwa  kizungu, wengi wenu mlinipuuza kwa sababu nilikuwa natumia  sheng. Hadi siku ile mligundua tuko na wafuasi wengi!!" alisema Femi.

IMEHARIRIWA NA D.OJIAMBO