Mwijaku azua madai kwamba Wasafi imekosa ubunifu

Muhtasari

•Kwa mara nyingine mwijaku amejitokeza na kueleza kuwa ubunifu wa   Wasafi  wa muziki unaendelea kudidimia kila uchao.

• Wasafi imesaini wasanii wengi ambao wameanza  kuonekana kuishiwa na ubunifu jambo ambalo limeanza kulemaza kazi ya lebo hio

Mtangazaji Mwijaku
Mtangazaji Mwijaku
Image: hisani

Kwa mara nyingine mwijaku amejitokeza na kueleza kuwa ubunifu wa   Wasafi  wa muziki unaendelea kudidimia kila uchao.

Mwijaku ambaye ni mtangazi wa kituo kimoja cha radio nchini Tanzani ameeleza kuwa wakati umewadia ambapo  Wasafi inafaa kuanza kuangazia lebo hio kwani mambo si sawa.

Alieleza  kuwa  Wasafi imesaini wasanii wengi ambao wameanza  kuonekana kuishiwa na ubunifu jambo ambalo limeanza kulemaza kazi ya lebo hio 

Alisema  wakati Wasafi ilikuwa ikianzia ilikuwa na uwezo mkubwa wa kuuza tiketi nyingi kuliko sasa jambo ambalo linaonyesha upetepetevu ulioko kwenye lebo hio.

Wasanii ambao wamesainiwa na Lebo ya Wasafi ni ; Zuchu, Ravyaan, Lava lava na  Queen Darling. 

Mwaka huu  wasanii ambao wameachilia   wimbo  na lebo ya hio , ni wawili tu, ambao ni Zuchu na  Ravyaan.

Mwijaku ameeleza kuwa msanii ambaye anajituma zaidi  ni Diamond kuhakikisha lebo hio inaendelea kwa kufanya  collabo na wasanii sifika ndani na nje ya nchi.

Isitoshe alitoa mfano kwamba wasanii ambao hawako kwenye lebo yeyote wameanza kuonekana kufanya vizur.