Imekwisha! Don Jazzy asema baada ya picha za ujauzito wa Rihanna na A$AP Rocky

Muhtasari

• Bosi wa rekodi lebo ya Mavin, Don Jazzy ameonekana kukubali matokeo baada ya picha za ujauzito wa msanii Rihanna na mpenziwe A$AP Rocky kuzagaa mitandaoni.

• Rihanna ambaye amekuwa mpenzi wa muda mrefu  wa Don Jazzy alionekana akiwa ubavuni mwake msanii A$AP Rocky katika matembezi jijini New York, Marekani.

Don Jazzy
Image: Instagram

Kinara wa Mavin Records, Don Jazzy ameonekana kukubali matokeo baada ya picha za ujauzito wa msanii Rihanna na mpenziwe A$AP Rocky kuzagaa mitandaoni.

Rihanna ambaye amekuwa mpenzi wa muda mrefu  wa Don Jazzy alionekana akiwa ubavuni mwake msanii A$AP Rocky katika matembezi jijini New York, Marekani.

Katika picha hizo ambazo zilichukuliwa huko Harlem, Rihanna anaonekana akiwa ubavuni mwa msanii A$AP Rocky huku akionekana mwenye furaha, amani na mtulivu huku akionyesha ujauzito wake bayana.

Wengi wa mashabiki wa Don Jazzy wamemjua kwa muda mrefu kuwa na mapenzi ya dhati kwa msanii Rihanna na inasemekana baada ya kuzisoma taarifa za ujauzito huo na pia kuona picha, Jazzy alivunjika moyo sana na kuweka picha za wawili hao kwenye mtandao wa Instagram akifuatisha na ujumbe “imekwisha”

Ikumbukwe taarifa za Rihanna kuwa na ujauzito wake wa kwanza kabisa zilivuja mitandaoni huku wengi wa mashabiki yake wakionekana kuwa na hisia mesto.

Wengine walimmiminia pongezi na kumhongera kwa kufanikiwa kuwa na ujauzito na kutarajia mtoto wake wa kwanza huku mashabiki wengine wakimkashifu kwa kubeba ujauzito na msanii A$SAP Rocky kinyume na matarajio ya wengi waliokuwa wanamjua kuwa mpenzi wa Don Jazzy.