Zuchu asema Diamond ni mwanamume mwenye mahaba tele

Muhtasari

•Zuchu kutoka lebo ya Wafasi  amemsifia bosi wake Diamond Platnumz kwa kueleza kuwa ni mwanamme anayejua kupenda na kuheshimu watu. 

•Amefunguka na kueleza mengi kuhusu ukaribu wake na bosi wake, huku akitaja alianza kupenda nyimbo za Diamond akiwa bado shule ya upili ambapo alikuwa anawaimbia wanafunzi kwenye tamasha mbalimbali.

ZUCHU
ZUCHU
Image: instagram/zuchu

Msanii kutoka Tanzania Zuhura Othman Soud almaarufu Zuchu wa lebo ya Wafasi  amemsifia bosi wake Diamond Platnumz kwa kusema kwamba ni mwanamume anayejua kupenda na kuheshimu watu. 

Kumekuwa na uvumi kuwa huenda msanii huyo akavishwa pete na bosi wake Diamond Platnumz siku ya Valentines.

Kupitia Mahojiano na kituo kimoja cha habari, Zuchu amefunguka na kueleza mengi kuhusu ukaribu wake na bosi wake, huku akitaja alianza kupenda nyimbo za Diamond akiwa bado shule ya upili ambapo alikuwa anawaimbia wanafunzi kwenye tamasha mbalimbali.

Kulingana naye, Diamond ni mwanamume anayejua kupenda na kutunza mpenzi wake, huku akitoa mfano wa mahusiano ya awali ya Diamond.

Alipoulizwa kuhusu wapenzi wa zamani wa Diamond; Hamisa Mobeto, Zari Hassan,Tanasha Donna, kama kuna mwenye anamkubali zaidi na angependa kuona wakiwa na  Diamond, Zuchu alisita kwa muda kisha akatoa maelezo yaliyokuwa tofauti na kile alichoulizwa, ingawa mwishowe alikubali ushauri wa wanahabari  kwamba Diamond anafaa abaki na yeye  na kufunga ndoa  .

Kinachosubiliwa sasa ni kuona kama siku ya wapendanao atabainisha mpenzi wake halisi ambaye alisema yuko nje ya nchi.