Mlinzi wa West Ham Kurt Zouma tabaani baada, Adidas yajiondoa

Muhtasari

•Mchezaji wa timu ya West Ham, Kurt Zouma amejipata pabaya baada ya kanda za video zilizomwonyesha akipiga  teke paka wake kwenye malazi yake.

 

Kurt Zouma
Kurt Zouma
Image: Hisani

Mchezaji wa timu ya West Ham, Kurt Zouma amejipata pabaya baada ya kanda za video zilizomwonyesha akipiga  teke paka wake kwenye malazi yake.

Zouma alisajiliwa na West Ham kutoka timu ya Chelsea ingawa kwa mkopo, tangu video hiyo kuonekana kwenye mitandao, wanamitandao wamekuwa  na maoni kinzani huku wengine wakitaka afikishwe mahakamani.

Siku ya Jumatatu  paka wawili ambao mchezaji huyo alikuwa amefuga nyumbani kwake walichukuliwa na shiriki la kulinda wanyama nchini Uingereza RSPCA. Hii ni baada ya picha kuonekana akimpiga teke mmoja wa paka wake.

Video ya Mfaransa huyo akimpiga teke paka wake ilisambazwa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii na kuvutia macho wapenzi wa wanyama na mamlaka  inayosimamia wanyama kuanza  kampeni za kumkashifu kwenye mitando ya kijamii.

Ingawa Kurt Zouma aliomba msamaha, timu ya West Ham imempiga faini kwa kosa alilotenda siku hiyo.

Kampuni ya vifaa vya spoti Addidas pia imeondoa ufadhili wake kwa mchezaji huyo kutokana na tukio hilo.

 Katika Taarifa Jumatatu, Jumuiya ya Kifalme ya Kulinda Wanyama ililaani kitendo cha Zouma huku ikibainisha kuwa wamemchukua paka hao.