KRG na Butita wamuangukia Mboya kwa msomo

Muhtasari

• Vincent Mboya, jamaa mwenye utata uliopitiliza ambaye alianza kugonga vichwa vya habari za burudani wakati alitangaza kurudisha alizosaidiwa na mchekeshaji Jalang’o

• Wasanii KRG the Don na Eddie Butita wakiongea na wakuza maudhui mbali mbali nchini walimpa msomo Mboya na mpaka kumkejeli kwamba ni maskini mwenye kiburi.

Mboya, KRG, na Butita
Image: Facebook

Vincent Mboya, jamaa mwenye utata uliopitiliza ambaye alianza kugonga vichwa vya habari za burudani wakati alitangaza kurudisha alizosaidiwa na mchekeshaji Jalang’o amepokezwa kipimo dhabiti cha msomo na KRG na Butita.

Mboya alikuwa gumza baada ya kutangaza kwamba alitaka kumrudishia Jalang’o kima cha shilingi elfu 18 ambazo mcheshi huyo alimsaidia baada ya Mboya kudai kwamba yuko na matatizo kibao.

Alisema kwamba alifikia uamuzi wa kurudisha pesa hizo baada ya Jalang’o kumpokeza kwa kejeli mno.

Februari 9, wasanii KRG the Don na Eddie Butita wakiongea na wakuza maudhui mbali mbali nchini walimpa msomo Mboya na mpaka kumkejeli kwamba ni maskini mwenye kiburi.

“Wewe namna gani wewe Mboya. Wewe enda huko bana hauna heshima. Tunaongelea mambo ya wasanii si watu kama wewe wenye wamechanganyikiwa. Shida yako ni uko na kiburi na ni maskani mshenzi. Wewe huwezi saidika. Ukisaidiwa na mtu, unakuja unatusi huyo mtu. Unajua huyo mtu alifanya kazi gani ndio akakusaidia?, halafu unakuja unamtusi kama unamdharau,” KRG the Don anaonekana akimsomea Mboya mbele ya kamera.

Kwa upande wake Butita amesema Mboya ni mshamba kwa asilimia 75 na ni taahira ambaye hayuko sawa kiakili.

Pia amemshauri kutafuta kitu anaweza fanya ili wasanii wengine waweze kumsaidia kusukuma kazi yake mbele badala ya kutafuta kiki za ugomvi na wasanii.

Lakini inaoenekama maneno haya ya KRG the Don na Eddie Butita kwa Mboya hayajachukuliwa vizuri na watu mitandaoni kwani wengi wameonekana kuwakashfu kwa kumdhalilisha kijana wa watu na kumuita maskini mshenzi.