Ravyanny na paula penzi lanoga siku ya wapendanao

Muhtasari

•Ravyanny  amewashangaza wengi baada ya kuvunja kimya chake kwa kuposti zawadi alizompatia mpenzi wake siku ya wapendanao.

 

Rayvanny na Paula Kajala
Image: Hisani

Mwanamuziki Raymond Shaban almaarufu Ravyanny  amewashangaza wengi baada ya kuvunja kimya chake kwa kuposti zawadi alizompatia mpenzi wake siku ya valentines.

Kupitia ukurusa wake wa instagram Ravyanny alipakia video fupi iliyokuwa ikionyesha zawadi alizompa mpenzi wake.

Kilichoashiria kuwa zawadi hizo zilikuwa za Paula Kajala ni kuwa Paula alikuwa amechapisha video hio kwenye  instastori yake.

Paula amekuwa akiposti picha za msanii huyo jambo ambalo mashabiki wamekuwa wakimtania kuwa aache kulazimisha mapenzi yake na Ravyanny na akubali kuwa aliachwa.

Wawili hao wamekuwa kwenye mitandao ya kijamii baada ya uvumi kuibuka kwamba wawili hao wameachana lakini kutokana na zawadi hizo bado mapenzi yako shwari.

Paula  Kajala anayesomea  chuo cha Uturuki ameoekana mwenye furaha isiyo na kifani huku akiposti picha za Rayvanny .