Bado hajakata tamaa ya kupenda - Amber Ray

Muhtasari

• Mwanamitindo Amber Ray amesema hawezi choka kupenda licha ya kuchezewa na wanaume na kisha baadaye kuachwa.

• Anayasema haya siku chache baada ya mwanamitindo huyo kufuta mchoro wa tattoo wa Jamal Rohosafi aliokuwa amechorwa mgongoni

Image: INSTAGRAM// AMBER RAY

Mwanamitindo Amber Ray amesema kwamba yeye bado ana Imani lazima atapenda tu na hawezi choka kupenda licha ya kuchezewa na wanaume na kisha baadaye kuachwa.

Anasema kwamba yeye kamwe hawezi kata tamaa katika suala zima la kupenda na kupata anayempenda eti kisa amechezewa sana na wanaume.

Amesema Imani yake hii inasukumwa sana na dhana kwamba moyo uko na sababu yake ya kutokuwa na mifupa.

“Sijui nani anafaa kusikia hili lakini mimi siwezi kosa kupenda tena eti kwa sababu nimetendwa mara kibao na wanaume. Kuna sababu mbona roho haina mifupa,” aliandika Ray

Mwanamitindo huyo anayasema haya siku chache tu baada ya aliyekuwa mume wake mfanyabiashara Jamal Rohosafi Marlow kurudi kwa mke mwenza ambaye ndiye mke wa kwanza, Amira.

Ray ameyasema haya siku ya wapendanao Februari 14 wakati anajivinjari na kujiburudisha mwenyewe baada ya kuachana na Jamal Rohosafi wiki kadhaa zilizopita.

Haya matamshi yake yanakuja siku chache baada ya mwanamitindo huyo kufuta mchoro wa tattoo wa Jamal Rohosafi aliokuwa amechorwa mgongoni na baada ya kutoa mchoro huo aliandika kwamba katu hajutii mapenzi aliyompa Jamal kwa sababu alijua fika kwamba aliyahitaji kipindi hicho.