Mamake Trio Mio afunguka kuhusu jinsi wanadada wamekuwa wakitongoza mwanawe

Muhtasari

•Mamake Trio Mio alisema kwamba wanawake wengi ambao wanammezea mate mwanawe wamekuwa wakipiga simu na hata kutuma picha zao tangu alipopata umaarufu.

•Trio Mio alikiri kuwa mara nyingi huwa anakabiliana na wanadada wengi wakati anapoenda kutumbuiza katika kumbi mbalimbali.

Trio Mio
Image: HISANI

Mama ya mwanamuziki mashuhuri TJ Mario almaarufu kama Trio Mio amefunguka kuhusu jinsi wanadada wamekuwa wakijipendekeza kwa mwanawe.

Akiwa kwenye mahojiano na Churchill, mamake Trio Mio alisema kwamba wanawake wengi ambao wanammezea mate mwanawe wamekuwa wakipiga simu na hata kutuma picha zao tangu alipopata umaarufu.

Mamake Trio Mio na ambaye pia ni meneja wake alifichua kwamba yeye ndiye hupokea jumbe na picha zinazotumwa kwani namba ya simu iliyowekwa kwenye kurasa za msanii huyo za mitandao ya kijamii ni yake.

"Huwa napata jumbe za sauti. Kuna wenye hutuma picha zao. Huwa najiuliza kama mimi ndio hutumiwa hizo, je kwa namba yake mwenyewe huwa anapata. Najua ni umri wake, yeye ni kijana" Alisema. 

Aliweka wazi kuwa mtoto huyo wa mwisho katika familia yake huwa anashauriwa kuhusu masuala ya maisha ikiwemo jinsi ya kukabiliana na wasichana. 

Kwa upande wake Trio Mio alikiri kuwa mara nyingi huwa anakabiliana na wanadada wengi wakati anapoenda kutumbuiza katika kumbi mbalimbali.

"Kwa mfano kuna shoo niliitwa na Mejja. Baada ya kufanya shoo manzi fulani alinirukia. Hata hivyo nilikuwa na walinzi wenye nguvu ambao walimtoa haraka. Muda uliisha alikuwa ashaondolewa" Trio Mio alisimulia.

Msanii huyo wa nyimbo za kisasa ambaye ana umri wa miaka 17 alisema atakuwa anamaliza shule baadae mwaka huu, hatua ambayo amesubiria kwa hamu kubwa.

Trio Mio
Image: HISANI