Ni kama nilifunga chapter ya kupata watoto- Carrol Sonnie afunguka

Muhtasari

•Mama huyo wa binti mmoja amesema huenda akajitosa kwenye mahusiano mengine siku zijazo ila kwa sasa hayuko tayari kuwa na mchumba.

•Muthoni ambaye amekuwa akiishi na mtoto wao pekee yake kufuatia utengano huo amekiri kuwa haijakuwa rahisi kuponya jeraha la moyo ila anandelea vizuri.

Image: INSTAGRAM// CAROL SONNIE

Aliyekuwa mpenzi wa mchekeshaji Mulamwah, mwigizaji Caroline Muthoni almaarufu kama Carrol Sonnie ameweka wazi kwamba hana wazo la kupata mtoto mwingine hivi karibuni.

Akishirisha mashabiki wake katika kipindi cha maswali na majibu kwenye mtandao wa Instagram, Muthoni alisema hajafunga moyo wake kupenda tena ila hajawazia kupata mtoto wa pili.

Mama huyo wa binti mmoja amesema huenda akajitosa kwenye mahusiano mengine siku zijazo ila kwa sasa hayuko tayari kuwa na mchumba.

"Sitaki kuwa na mchumba kwa sasa, labda siku zijazo. Kwa watoto, nikama nilifunga hiyo chapter!" Muthoni alijibu shabiki aliyetaka kujua kuhusu mpango wake wa mahusiano na watoto.

Mwigizaji huyo na aliyekuwa mpenzi wake Mulamwah walitangaza kutengana kwao mnamo mwezi Desemba mwaka jana, takriban miezi mitatu tu baada ya kubarikiwa na mtoto wa kike, Keilah Oyando.

Muthoni ambaye amekuwa akiishi na mtoto wao pekee yake kufuatia utengano huo amekiri kuwa haijakuwa rahisi kuponya jeraha la moyo ila anandelea vizuri.

"Sio lazima upone hasa kama kuna mtoto aliyehusika. Lakini kadri siku zinavyosonga mambo hufunguka" Muthoni aliambia shabiki aliyetaka kujua jinsi alivyosonga mbele na maisha baada ya mahusiano kugonga mwamba.

Muthoni amesema atazungumzia kiini cha mahusiano yake na Mulamwah kuvunjika wakati mwafaka utakapofika.

Hivi majuzi Mulamwah alifichua kuwa kuna mambo mengi ambayo yalipelekea kutengana kwao ikiwemo kutofautiana kuhusu matumizi ya pesa.