Diana Marua amsherehekea binti ya aliyekuwa mpenzi wa Bahati, Yvette Obura

Muhtasari

•Diana Marua amempongeza msichana huyo mwenye umri wa miaka sita kwa mafanikio hayo ya kielimu.

•Yvette alisema bintiye alimtishia babake Bahati , mashangazi wake na wanafamilia wengine kuwa wangekosana iwapo wangekosa kuhudhuria.

Image: INSTAGRAM// YVETTE OBURA

Binti ya Bahati na mpenzi wake wa zamani Yvette Obura, Mueni Bahati anahitimu leo (Ijumaa) kuingia darasa la kwanza.

Mke wa sasa wa mwanamuziki huyo, Diana Marua amempongeza msichana huyo mwenye umri wa miaka sita kwa mafanikio hayo ya kielimu kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Diana ambaye hivi majuzi alizindua taaluma yake ya muziki akijitambulisha kama rapa Diana B amesema kuwa anajivunia binti huyo wa kwanza wa mumewe.

"A Girl Toto, mtoto wa malkia @mueni_bahati anahitimu leo. Hongera sana mtoto wa kike, tunajivunia wewe. Hugs na mabusu kutoka kwa Aunty Dee" Diana aliandika.

Hapo awali Yvette alikuwa ameichua kuwa binti yake alikuwa amekuwa amepigia wanafamilia wa karibu simu akiwaalika kwenye hafla ya kuhitimu kwake.

Yvette alisema bintiye alimtishia babake Bahati , mashangazi wake na wanafamilia wengine kuwa wangekosana iwapo wangekosa kuhudhuria.

"Ni msimu wa kuhitimu kwa shule ya awali. Mueni amempigia simu babake, shangazi zake, na familia nzima moja kwa moja ili tu kuwaambia waache wanachokifanya hivyo kesho na kuhudhuria kuhitimu kwake. Anamaliza kwa 'ukikosa tutakosana' nakufa" Yvette alisema.

Licha ya kutengana kwao miaka kadhaa iliyopita, Yvette na Bahati wameendelea kushirikiana vizuri katika ulezi wa binti huyo wao.