Nicky Bigfish afurushwa kutoka nyumba ya kupanga kwa kuwadhihaki wenye nyumba na caretakers

Muhtasari

•Barua ambayo mchekeshaji huyo alionyesha kwenye ukurasa wa Instagram inaashiria kuwa anahitajika kuwa amehama nyumba yake iliyo Kilimani kabla ya Aprili 7, 2022.

•Mchekeshaji huyo pia amefahamishwa kuwa atakatwa 40,000 za kupaka nyumba yake rangi upya.

Image: INSTAGRAM// NICKY BIGFISH

Mchekeshaji mashuhuri Nicky Bigfish huenda akalazimika kutafuta makao mapya baada ya mjasiriamali aliyemkodisha nyumba kutoridhishwa na video yake ya utani ambayo alitengeneza hivi majuzi.

Barua ambayo mchekeshaji huyo alionyesha kwenye ukurasa wa Instagram inaashiria kuwa anahitajika kuwa amehama nyumba yake iliyo Kilimani kabla ya Aprili 7, 2022.

Mwenye nyumba wake  amemshtumu kwa kuwadhihaki wamiliki nyumba na wasimamizi wa katika video yake ya hivi majuzi na kudai kuwa inachochea wapangaji kuwadhalilisha wasimamizi wa manyumba yao.

"Tungependa kukujulisha kuwa unapaswa kuhama ndani ya kipindi cha siku 30 zijazo kutoka leo. Hii ni baada yetu kuona video ambayo imekuwa ikienezwa kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo kikundi cha WhatsApp cha makao haya ambapo uliwadhihaki na kuwachezea mzaha wasimamizi na wamiliki nyumba. Maoni yetu ni kuwa video hiyo inalenga kuwachochea wapangaji kuchelewesha kodi na kuwadhalilisha maajenti wetu. Tafadhali hama katika kipindi ulichopewa na uache kila kitu ulivyopata,"  Barua hiyo ilisoma.

Mchekeshaji huyo pia amefahamishwa kuwa atakatwa 40,000 za kupaka nyumba yake rangi upya.

Hizi baadhi ya hisia za Wanamitandao;

djshiti_comedian: Mbleina

tony_mwirigi: Bro hawa wasee kwani hawajui wewe ni msanii na ni beshte ya DJ Shiti?

africancastro: Anajua soon utakuwa landlord, usikufe moyo