Alikiba atembelea familia yake Mombasa, je wamerudiana?

Muhtasari

• Alikiba aonekana na familia yake, watu wahisi amerudiana na mkewe baada ya fununu za talaka.

Ali Kiba na mkewe Amina
Ali Kiba na mkewe Amina
Image: hisani

Siku chache zilizopita, video ya msanii wa Bongo Fleva, Alikiba akiwa na muda maalum na familia yake jijini Mombasa iliacha wengi wakizungumza kuhusu uwezekano wa Kiba na mkewe Amina kutatua ugomvi wao uliozua fununu za kuvunjika kwa ndoa yao.

 Wengi wa mashabiki wa staa huyo walifurahia sana video hiyo ilizosambazwa kwa wiki mitandaoni ikimuonesha Alikiba akicheza na wanawe wawili katika maeneo ambayo yalikaa ya Kimombasa hivi. 

Mwezi jana kulikuwa na fununu kwamba mkewe Alikiba Amina Khaleef alielekea mahakamani ili kuomba talaka yake kutoka kwa staa huyo kwa kile alichokitaja kuwa ni unyanyasaji wa matusi, na kukatishwa tamaa kutoka kwa wakwe miongoni mwa masuala mengine.

Fununu hizi hata zilitiwa nguvu zaidi na ujumbe ambao msanii huyo aliandikia mwanawe akimtaka asimsahau ambao wengi waliutafsiri kuwa ni wa huzuni na msanii huyo amesalimiwa na ukweli kwamba wanatengana na familia yake na hivo ataikosa kampani ya watoto wake.

Video hiyo ambayo imepakiwa na mashabiki wengi wa msanii huyo inaashiria kama mwamko mpya vile ambapo anaonekana akiwa amembeba mmwanawe mmoja begani na kwa umbali inasikika sauti ambayo inaaminika kuwa ya mkewe Alikiba.

Watu wamekuwa wakiichambua video hii utadhani karanga, wakidai kwamba hii ni ishara ya kiutu uzima ambapo huenda hatimaye Alikiba na mkewe wametumia busara na kuyatatua nje ya mahakama ya kadhi na pengine wameafikia uamuzi wa kuendeleza gurudumu la ndoa yao baada ya minong’ono mingi kwamba wataachana.    

Msanii huyo alifunga ndoa ya kufana mwaka wa 2018 katika pwani ya Kenya ambapo alishabikiwa na wengi kwa hatua hiyo ya ujasiri ambayo imewashinda wasanii wengi wakubwa wenye haiba yake ambao wameishia kwa kuchepuka tu.