Ugomvi wangu na Alikiba uliisha, sisi ni marafiki - Shilole

Muhtasari

• Muigizaji na Msanii Shilole ameweka wazi kuhusu tofauti zake na Alikiba na kusemac kwamba ugomvi huo uliisha na wanatazamia kufanya kazi pamoja.

Alikiba, Shilole
Image: Maktaba

Muigizaji na msanii Shilole akizungumza katika vyombo vya habari nchini Tanzania ambapo alikuwa katika ‘media tour’ ya kuutambulisha wimbo wake mpya wa Mama Ntilie, alisema kwamba walimaliza ugomvi wao na Alikiba kwa njia ya kistaarabu na kusema kuwa ni marafiki wakubwa.

Shilole na Alikiba wamekuwa wakitupiana maneno katika vyombo vya habari na mitandaoni kwa muda sasa ambapo Alikiba alikuwa anasema hakumualika Shilole kwenye uzinduzi wa albamu yake.

Katika mojawapo ya mahojiano kwenye ziara yake hiyo kwenye vituo vya habari, Shilole aliulizwa swali hilo na kusea kwamba walimaliza ugomvi wao na Alikiba na urafiki ukarejea.

“Kupatana ni vizuri kwa sababu maisha ni mafupi hapa duniani. Mashabiki wategemee kuona kazi zangu na Alikiba siku zijazo,” alisema Shilole.

Kwa kudhibitisha hilo, Shilole alipakia kwenye instastories zake video yake ya Mama Ntilie ambayo msanii Alikiba alikuwa ameiweka kwenye ukurasa wake kama njia moja ya kutoa sapoti kwa mwanadada huyo.

Tamko hili la kusameheana linakuja wakati ambapo mtangazaji Mwijaku anaiua madai kwamba Shilole alifaa kuwa mke wa Alikiba na wala hamchukii mume wake wa sasa ila angetaka kumkuambia Shilole aolewe na Alikiba kama mke wa pili, hangekataa na wala hata Alikiba hangelipinga hilo.