"Ninafurahia ngono na wanawake lakini sisisimki, navutiwa na wanaume, mimi ni shoga?" mwanaume atafuta ushauri

Muhtasari

• Mwanaume huyo alitafuta ushauri kwa daktari kusaidiwa kutambua jinsia yake.

• Alidai huwa anafurahia tendo la ndoa na wanawake lakini kila anapotembea nje hujipata kuvutiwa na wanaume.

Mwanaume aliyevunjika moyo wa mapenzi
Mwanaume aliyevunjika moyo wa mapenzi
Image: THE STAR, MOSES SAGWE

Mwanaume mmoja ni mtu mwenye wasiwasi wa kujitambua kijinsia baada ya kudai kwamba ameshindwa kujitathmini kikweli kama yeye ni mtu wa kawaida ama ni mtu mwenye fikira, mawazo na mvuto wa kundi la LGBTQ.

Mwanaume huyo alifichua hayo kwa daktari mwanasaikolojia wa masuala ya maisha ya ngono ya binadamu nchini Marekani ambapo alidai kwamba kwa kawaida huwa anafurahikia sana kufanya tendo la ndoa na watu wa jinsia ya kike lakini muda wote huwa anajipata akiwafikiria sana wanaume anaowaona.

Akielezea matukio hayo yanayomkumba kila mara, alitaka daktari huyo amsaidie kujitambua kama kweli yeye ni mtu wa kawaida ama ni shoga ambaye hajajitambua.

“Mimi ni mwanamume mwenye umri wa miaka 22 na nimechanganyikiwa sana kuhusu jinsia yangu. Sijui kama mimi ni shoga, mtu wa kawaida au mtu mwenye jinsia mbili. Nimefanya ngono na wanawake na ninaifurahia, lakini kwa ujumla sijipati kusisimka sana. Nina wasiwasi naweza kuwa shoga, ingawa: Wakati mwingine mimi hupata ninafikiria kuhusu wanaume, na kuwatazama ninapokuwa nje matembezini. Nimetazama ponografia ya mashoga na hainiwashi. Wala ngono za wasagaji hazifanyi kazi - ponografia ya kawaida baina ya msichana na mvulana pekee ndio hunisisimua. Tafadhali nisaidie - hili limekuwa tatizo linaloendelea tangu nilipokuwa na umri wa miaka 16 na ninapata shida kila siku. Nataka tu kujua mimi ni nani!” alieleza kwa wasiwasi mwanaume huyo.

 

Daktari huyo akimshauri, alimuambia kwamba aache wasiwasi kwani bado yupo katika umri mbichi sana kama jani la mgomba katika suala zima la kujitambua katika maisha ya tendo la ngono. Alimwambia kwamba watu wengi tu huwa na wasiwasi kama huo wa kuchanganyikiwa katika kujitambua kijinsia kwa muda mrefu.

Daktari alimshauri ajaribu sana kujiepusha na fikira hizi za kijamii kuhusu hisia za kingono na badala yake kuzingatia katika kujibu hisia zake namna hiyo kwa mtu yeyote pindi zinapoibuka.

Pia alimuusia kujikubali na kukubali kutangamana na watu wa kweli ili kujitambua bila kujihukumu au kuogopa kuhukumiwa na watu na wala si kutangamana na video za kingono.

 

Bila shaka vijana wengi tu waliobaleghe hujipata katika njia panda kama hizi kushindwa kuzitambua hisia zao za kingono na pasi na ushauri wa mapema wengi hutumbukia katika shimo la ushoga na usagaji.