"Upuuzi mtupu, si mimi niliandika!" Betty Kyallo akanusha maneno kuwa alishauri wanadada kuchumbiana na 'sugar daddies'

Muhtasari

• Betty Kyallo amekana nukuu inayosambazwa mitandaoni kwamba ni yeye alitoa ushauri wanawake kuchumbiana na watu wenye pesa na kuachana na wanaume maskini.

Betty Kyallo
Image: Instagram

Mwanahabari maarufu wa runinga Betty Kyallo sasa ameweka bayana kuhusu madai ambayo yamesambaa pakubwa mitandaoni yakidai kwamba alisema hawezi chumbiana na mwanaume kabwela.

Kupitia instastories zake, Kyallo amepakia sehemu ya ujumbe huo unaodaiwa kuwa ni maneno yake yaliyonukuliwa na kusema kwamba matamshi hayo si yake na kuyapuuzilia mbali.

“Nina viwango. Siwezi chumbiana na mwanaume ambaye hana gari zuri, gari zuri maana yake ni TX au V8. Nikichumbiana na mwanamume anayemiliki probox, basi ni kama kutukana viwango vyangu. Siwezi kumpenda mwanaume ambaye analipwa mshahara mdogo kuliko mimi na hana gari bora kuliko mimi. Nawasihi wanawake wenzangu kuweka viwango, bora, chumbiana na sugar daddy kuliko hawa wavulana wanaohangaika kupumua,” maneno hayo ambayo Kyallo ameyapuuzilia mbali yalisema.

Mwanahabari huyo ameyakana vikali maneno hayo kwamba hayakutoka kwake na kuwataka mashabiki wake kutoamini kila kila ambacho wanakisoma kwenye mitandao ya kijamii.

“Upuuzi mtupu. Bandia,” Betty Kyallo aliandika akifuatisha na picha na nukuu hiyo iliyodaiwa kutoka kwake.

Alisema kwamba ni wakati sasa watu wakome kuamini kila walisomalo kwenye mtandao kwa sababu yeye siku zote amekuwa ni mtu wa kutetea jitihada na bidi, na si kitu kingine kama kuwashauri wanadada kuchumbiana na watu wenye pesa.

“Msiamini kila kitu mnachokisoma kwenye mtandao. Sisi sote ni lazima tujitume kwa bidi kwqa sababu hakuja jambo rahisi hapa nje. Hicho ndicho kitu ambacho siku zote nimekuwa nikisisitiza, BIDII,” aliandika Kyallo kwenye instastories yake.

Pia alizidi kusema kwamba jitihada ya kila mtu hata kama ni ndogo inahitaji kupewa hongera na kushabikiwa kwa sababu kila mtu lazima aanze na mahali fulani kabla ya kuinukia kwenye umaarufu na vitu vingine vizuri.

“Pia, jitihada ya kila mtu sharti isherehekewe kwa sababu naamini kila mtu kuna mahali anaanzia na kukwea ngawzi pole pole,” aliendelea kuandika Kyallo.

Mwanahabari huyo alionesha wazi kugadhabishwa kwake na mtu au mwanablogu anayetumika jina na picha zake kujifanya yeye na kuandika kauli za kupotosha mitandaoni watu wakidhani ni Kyallo mwenyewe. Alisema wale wanaofanya hivyo wanatafuta riziki lakini kwa njia mbaya.

“Lakini pia naelewa watu sharti wakarabati hadithi bandia ili kupata riziki na wengine hufanya hivyo ili kutafuta kiki mitandaoni. Kwa taarifa yeenu mimi magari hata hayanivutii,” alimaliza Kyallo na kuwatakia mashabiki wake siku njema.