"Alinicheat nikahakikisha amepata UKIMWI kupitia rafiki yangu mwathirika" Mwanamke asimulia

Jibu hilo lilikuja baada ya GK Nyambura kuuliza nini watu wamewahi fanyia wapenzi wao wa zamani.

Muhtasari

• Mwanamke huyo alieleza kwamba baada ya mpenzi wake kuchepuka, alilipa kisasi kwa kuunganisha rafiki yake mwathirika wa Ukimwi na yeye na kumuambukiza.

Mchoro wa ukimwi
Mchoro wa ukimwi
Image: The Star

GK Nyambura, mwanadada ambaye amejizolea umaarufu baada ya video fulani kusambaa ikimuonesha alivyojitoma kwenye nyuma na mpenzi wake wa awali saa za alfajiri ili kuchukua vitu vyake vilivyosalia mule kipindi wakiwa katika mapenzi juzi kati aliuliza swali kwenye ukurasa wake wa Instagram ambao majibu yake yalikuwa ya kuchekesha na kusikitisha mno.

Ilianza tu pale ambapo Nyambura aliuliza kwenye instastory yake akitaka watu kufungua roho kuhusu kitu kibaya zaidi ambacho waliwahi kifanya kwa wachumba wao.

Wanawake wengi ndio walionekana kuachia majibu ya kustaajabisha kuhusu vitendo ambavyo waliwahi wafanyia wapenzi wao, huku baadhi wakisema walidanganya mambo mbali mbali.

“Nilizima simu yake na kuificha sehemu ambapo hangeweza kuipata na kishqa nikapigia wazazi wake simu kuwataarifu kwamba mwanao amekufa,” mmoja alijibu bila soni.

Kwa kuificha simu ya mtoto wa watu, bila shaka watu wa kwao huenda waliamini ‘kifo’ chake kwa sababu walijaribu kumtafuta na hakupatikana kwa simu. Aisee huyu alifanya mzaha na suala la kifo.

Ila pia katika baadhi ya majibu ambayo GK Nyambura alipakia kwenye msururu wa instastories zake ni kisa kimoja cha mwanadada aliyesema kwamba alikuwa katika mahusiano na mvulana mmoja baada ya kuachana kwa kile alidai huyo mvulana alichepuka, mwanadada alihakikisha kwamba kijana wa watu amepata virusi vya UKIMWI kama malipo ya kuchepuka kwake.

“Nilihakikisha nimemuunganisha na Rafiki yangu ambaye ni mwathirika wa virusi vya UKIMWI nikahakikisha amemuambukiza na kisha baadae kumuacha, hiyo ilikuwa kama kisasi kwa kuchepuka,” mwanadada huyo alisema.

Hili lilistaajabisha wengi ambao walisema kwamba kweli wanawake ni watu wabaya sana katika kulipa kisasi maana malipizi yao huacha donda la maisha katika nafsi ya mtu.

Jibu hilo lilizua mjadala mkali kwenye mtandao wa Twitter ambapo wengi walisema wanawake wengine ni mashetani sana kuvuruga maisha ya watu kisa kuchepukiwa tu.