"Sioni maana ya kuishi mwangu ukiwa futi 6 ardhini" Ngotho aliomboleza mwanawe kabla ya kufa

Cecy Ngotho alipoteza mwanawe miezi miwili iliyopita kabla ya kutumbukia kwenye mtaro wa ujenzi wa barabarani.

Muhtasari

• Ngotho alionekana mwenye mawazo mengi tangu kumzika mwanawe, kupitia jumbe za huzuni alizokuwa akipakia kwenye Facebook.

• Inaarifiwa alipatikana amefariki baada ya kushindwa kustahimili machungu ya kumpoteza mwanawe wa kipekee.

Cecy Ngotho na mwanawe kabla ya kifo chake
Cecy Ngotho na mwanawe kabla ya kifo chake
Image: Facebook//Cecy Ngotho

Jumatatu mwanahabari Mike Nyagwoka aliachia ujumbe weney ukakasi mkubwa kumuomboleza mmoja wa rafiki zake mkubwa ambaye inasemekana alipatikana amekufa, miezi miwili tu baada ya kumpoteza mwanawe.

Katika ujumbe huo, Nyagwoka alisema mwanadada huyo alikuwa anapitia waakti mgumu sana kwa kumpoteza mwanawe kwa ajali ambapo aligongwa kichwa chake kwa kuanguka kwa mtaro wa ujenzi wa barabarani na tangu kumzika, amekuwa na unyongovu na msongo wa mawazo, jambo ambalo huenda lilisababisha naye kufa.

“Mnamo Juni 5, 2022, mwanangu aligonga kichwa chake dhidi ya mtaro kutoka kwa ujenzi wa barabara unaoendelea katika eneo la Kidfarmaco, Kikuyu tunakoishi. Alikufa papo hapo kutokana na kuvuja damu kwa ndani. Kumzika mtoto wako ni ndoto mbaya zaidi nisingependa hata kwa adui yangu, maumivu hayaelezeki,” aliandika mwanamama huyo kumuomboleza mwanawe.

Taarifa za kifo cha mwanamke huyo aliyetambulika kama Cecy Ngotho zilisambazwa pakubwa mitandaoni huku ujumbe wa mwisho ukiibuka ambao aliandika kuonesha alikuwa anapitia hali mbaya ya msongo wa mawazo, wengine walisema kwamab alipatikana amefariki kwa kujiua.

“Leo ni siku 40 tangu ulipoota mbawa. Hakuna kitu kimekuwa sawa, maumivu ya mara kwa mara katika moyo wangu yanazidi kuwa mabaya kwa kila dakika. Sijaweza kukubaliana na hasara hiyo na ninaendelea kutazama nje, nikitumai kuwa utarudi. Sehemu nzuri zaidi ya mimi ilikufa siku uliyopofariki. Nataka kuamka kando yako kama ulivyokuwa ukifanya siku zote,” Ngotho aliomboleza mwanawe katika ujumbe wa kuliza aliopakia kwenye Facebook yake.

Alidokeza kwamba hana furaha kabisa katika maisha haya akijua kwamba mtoto wake wa kipekee yupo futi sita ardhini na kusema hakuona ladha ya maisha tena pasi na mwanawe.

“Nachukia sana mawazo ya kwamba mimi ninaishi wakati wewe mwanangu upo futi sita ardhini. Nimekukosa sana mwanangu. Ulikuwa ulimwengu wangu, kibeti changu. Sioni maana yoyote ya kuendelea kuishi,” ujumbe wake wa mwisho ulisoma.

Nyagwoka alidokeza kwamba alitaarifiwa Ngotho alipatikana amekufa baada ya kuonekana mwenye mawazo mengi kupitia jumbe alizokuwa akiziachia kwenye mitandao yake, siku kadhaa baada ya kumpoteza mwanawe.