Diana Marua: Tutatangaza jinsia ya mtoto wetu kesho mchana

Marua anatarajiwa kujifungua siku chache zijazo kwani tayari miezi tisa imeshatimia.

Muhtasari

• Marua ametangaza kufichua jinsia ya mwanawe mtarajiwa kesho Jumanne saa tisa .

• Mke huyo wa Bahati anatarajiwa kujifungua wiki hii.

Bahati na mke wake Diana Marua

Mpenzi wake mwanamuziki Kevin Kioko almaarufu Bahati, Diana Marua alisema kuwa  watatangaza jinsia ya mtoto wao wanayemtarajia kesho Jumanne.

Katika ukurasa wake wa Instagram, mwanablogu huyo aliwauliza mashabiki wake ikiwa wanatarajia mtoto wa kiume ama wa kike.

Marua alifichua hilo baada ya kurudi kwenye mtandao wa YouTube baada ya muda mrefu wa kupotea.

"Tutatangaza jinsia ya mtoto wetu kesho saa tisa kamili," mkewe Bahati alitangaza.

Mama huyo wa watoto wawili na mmoja mtarajiwa alikuwa amedokeza kujifungua leo baada ya kusema kuwa amehitimiza miezi tisa ya kuwa mja mzito.

Alikuwa amesema alivyokuwa akihisi uchungu wa uzazi siku hiyo na likuwa na matumaini ya kujifungua.

Marua alikuwa ameeleza jinsi ujauzito huo umekuwa na changamoto nyingi na kuwa umekuwa safari ndefu.

Alisema kuwa ujauzito huo ulimfanya asijiweze kwa siku za mwisho kabla ya kujifungua kwa kuwa ilikuwa ngumu kwake kutembea, kutoka kitandani na hata kuvaa viatu.

"Imekuwa safari ndefu, kuna wakati ambao maisha yalikuwa nyororo, ambapo sikuwa napenda pua langu lilivyokuwa dogo, ambao nilikuwa natembea vizuri na si kama ..., ambao kugeuka kitandani na kulala kifudifudi," Marua alieleza safari ya uja uzito wake.

Aliongeza kuwa alikuwa hawezi kuvaa kiatu akiwa na ujauzito wake kwa kuwa miguu yake ilikuwa imefura mithili ya ndovu.

Hata hivyo, mashabiki walimtakia safari njema ya kujifungua.