(+video) Mtoto abusu picha ya marehemu babake na kumwambia kwaheri, video yawaliza watu

Mtoto huyo mdogo alionekana akiibusu picha ya marehemu babake aliyezikwa mwezi mmoja uliopota huku akimpungia mkono wa buriani.

Muhtasari

• Mtoto huyo anasikika akiulizwa huyo ni nani ambapo anasema kwa madaha kwamba ni babake mzazi huku akiibusu.

Katika upeo wa dunia, unaambiwa wazazi ndio Miungu wa pili, lakini usiwaabudie! Hakuna kitu ambacho kinapendeza na kulainisha maisha ya mtoto yeyote yule akiwa anakulia maisha yenye uwepo wa wazazi wake.

Ila kwa wale amabo wanakosa bahati ya kutowaona wazazi wao, huwa ni majonzi makubwa kwa upande wao, ila kwa mtoto mdogo, hawezi fahamu mpaka akue.

Kuna video moja ambayo ilipakiwa kwenye mtandao wa Facebook ikimuonesha mtoto mmoja mdogo akiibusu picha ya marehemu babake na kumpa buriani.

Video hiyo ambayo imewaliza wanamitandao wengi inamuonesha kijana huyo mdogo kwa furaha ya kitoto akiwa anaibusu picha ya marehemu babake mara kadhaa na ikielekea kumalizika anaonekana akimpungia mkono wa kwaheri ya kuonana.

Kanda hiyo ilipakiwa na anayedaiwa kuwa mama wa mtoto huyo, Bonny Lazaro kwenye mtandao wa Facebook na inaonyesha mvulana huyo akibusu picha ya ukumbusho wa baba yake kwa njia nzuri zaidi, jambo ambalo limeibua hisia za majonzi kutoka kwa wanamitandao.

Katika maandishi yaliyoonekana kwenye picha hiyo, babake mtoto huyo alifariki mwezi mmoja uliopita na watu wanasikika wakimuuliza kijana huyo kuhusu utambulisho wa picha hiyo ambapo anajibu kwamba ni babake.

Kwa kuzingatia klipu hiyo, mvulana huyo alikuwa anampenda baba yake kwani hakutaka kuiweka picha hiyo chini au kuiondoa machoni mwake. Dada yake mkubwa pia alionekana akibusu picha hiyo kabla ya video kuisha.

Kitendo hicho cha mtoto huyo mdogo kuibusu picha ya babake huku akimpungia mkono wa buriani iliwaliza wengi ambao walitolea maoni yaliyoashiria huruma na majoniz kwa wakati mmoja.

Katika msururu wa machapisho amabyo mwanamke huyo amekuwa akipakia kwenye ukurasa wake wa Facebook, anaonekana kujawa na simanzi huku akidokeza kwamba alimzika mumewe tarehe mosi Oktoba na tangu hapo maisha yake hayajarejea sawa.

“Nilimzuka mume wangu tarehe moja Oktoba, mpaka sasa ninahisi nimeganda, mwili wangu umekufa nusu. Nina hasira kwa Mungu. Hakuna maneno mengi yanayonifanya nijisikie vizuri zaidi! Njeeeeeee nahisi ningekufa vilevile pamoja na watoto wetu niende nao,” mwanamke huyo aliandika kwa majonzi.