(+Video) Kinyozi atumia vifaa vya hisabati kunyoa wateja

Kinyozi huyo alitumia zana za kiufundi za kuchora kama rula na dira alipokuwa akipima kichwa cha mteja wake kabla ya kumnyoa.

Muhtasari

• Watu wengi walitaka kujua iwapo kinyozi huyu alikuwa mwalimu wa zamani lakini baadaye akawa mhudumu wa kinyozi.

Kinyozi atumia rula na dira kuwanyoa wateja wake.
Kinyozi atumia rula na dira kuwanyoa wateja wake.
Image: TikTok/@zakmwash

Kinyozi mmoja nchini Nigeria aliwafanya watu wengi kuzungumza kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuonekana kwenye video akinyoa wateja wake kwa vifaa vya hisabati.

Katika video hiyo ambayo ilisambaa kwenye mtandao wa TikTok, kinyozi huyo alitumia vifaa vya hisabati vya kuchora kama rula na dira alipokuwa akipima kichwa cha mteja wake kabla ya kumnyoa.

Video hiyo iliwafanya watu wengi kuwa na maswali mengi akilini mwao huku wakishangaa iwapo kinyozi huyo alikuwa mwalimu wa hisabati hapo mwanza au pengine kazi ya mwalimu ilimpiga chenga akaamua afungue kinyozi.

Klipu hiyo iliyopata watazamaji wengi, walioiona waliashiria kutamani sana kunyolewa kwa ufundi huu na wengine wenye biashara kama hii kuonekana wakitaka kufunzwa ustadi huu wa kipekee.

"Unapokuwa mwanahisabati lakini mambo yanaharibika na kufungua kinyozi, ili uendelee kuishi." Vendetta 86 alisema.

''Kwa nini naona video hii mara kwa mara? hii ni mbinu mpya'' Mashhud alishangaa

 "Je, Huku ni kuchora kwa aina ngani? Nimependezwa nayo." ebiskiti alisema.

"Ulihitaji nini ili kufanya haya yote kaka?." ubogokenneth aliuliza.

 "Huyu jamaa ni stadi wa jiometri." Keith Lypn White alisema.

 "Hii ina maana kwamba yote tuliyojifunza shuleni sio bure.'' OBEYAWAH alisema.

"Ni kama kinyozi huyu alihitimu kutoka Chuo Kikuu cha vinyozi na na cheti cjha PHD katika hisabati ya juu." Niz Blanchard alitania.

 "Kwa hivyo kukata nywele kunastahili ujuzi pia?." Lihleithuba alitaka kujua.