Diana Marua amwandikia mumewe Bahati ujumbe mtamu huku akisubiri kujifungua

Marua alimshukuru mume wake kwa kuitunza familia yao yote.

Muhtasari

• Marua alimsifia Bahati kuwa baba na mume bora kwa kuwatunza na kuwasimamia kama mkubwa wa familia yao.

Bahati na Diana Marua

Mwanavlogu  Diana Marua amemwandikia mume wake  Bahati ujumbe mtamu wa mahaba kumueleza  jinsi anavyompenda.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diana aliusifia muonekano wa baba huyo wa watoto wake wawili.

"Daamn, huyu ndiye Mfalme wangu , baba ya watoto wangu," aliandika.

Alimshukuru Bahati kwa yote ambayo amekuwa akifanya ili kuhakikisha kuwa yeye na watoto wao wako sawa.

Rapa huyo alimpa mumewe motisha wa kuendelea kufanya kazi yake kwa bidii ili  waendelee kufanikiwa zaidi.

Alisema ana imani kuwa mwanamuziki huyo ataendelea kufanikiwa katika kazi yake ya kuwa mwanamuziki.

"Nakushukuru Mungu kwa mpenzi wangu. Mungu abariki mienendo yako na mwelekeo wako. Mungu azidi kuibariki kazi ya mikono yako na kupa mapendeleo na faraja kwa binadamu kila siku ya maisha yako," aliandika.

Wanandoa hao wanatarajia mtoto wao watatu baada ya kuwa kwenye ndoa kwa miaka kadhaa.

Rapa huyo mjamzito aliandika ujumbe huo baada ya kuonyesha dalili za kukaribia kujifungua alipopakia video iliyoonyesha akiwa hospitalini.

Leo Jumanne, Diana alitangaza kuwa mazingira hayo ya hospitalini ndiyo yake kwa sasa hadi pale atakapojifungua.

Siku za hivi karibuni Marua amekuwa akidokeza kujifungua hivi karibuni.

Takriban wiki mbili zilizopita, wanandoa hao walitangaza kuwa wanatarajia mtoto wa kike ila walikuwa wamekisia kupata mtoto wa kiume.