Bahati afichua sababu ya kukawia kufanya harusi

Mwanamuziki huyo alifichua haya baada ya kutangaza kufanya harusi hivi karibuni

Muhtasari

• Mwanamuziki huyo alisema kuwa anapenda hafla za kifahari na angependa harusi yake na Diana kuwa ya kifahari.

Image: INSTAGRAM// BAHATI KENYA

Mwanamuziki Kevin Kioko almaarufu Bahati alifichua kuwa atafunga pingu za maisha na mkewe Diana Marua hivi karibuni.

Katika sherehe ya kufichua jinsia ya mtoto wanayetarajia, mwanamuziki huyo alisema kuwa anapanga harusi kubwa ya kifahari.

Alifichua sababu yake ya kukawia kufanya harusi baada ya kuchumbiana na mkewe kwa miaka mingi na kusema kuwa hangetaka kufanya harusi ndogo.

"Unajua mimi ni mtu anayependa kufanya mambo kwa kuongeza ladha, nikiandaa hafla napenda kuandaa hafla kubwa," Mwanamuziki huyo alisema.

Bahati alifichua hili baada ya kumwandalia mkewe Diana sherehe ya kufichia jinsia ya mtoto wao.

Sherehe hiyo iliyoandaliwa ilikuwa ya kifahari ambayo Diana hakutarajia.

"Nimekulipia chumba cha kifahari kabisa katika hoteli hii. Hapo ndipo utakapolala leo,kama zawadi yako,"' Bahati alimwambia mkewe.

Alisema kuwa baada ya sherehe hiyo, jambo litakalokuja baadaye ni harusi yao na amepanga kuwaalika waliohudhuria sherehe yao.

Mwanamuziki huyo amekuwa akionekana kuwa mwanamume anayependa kumzawadi mkewe kwa vitu vya thamani na vya kifahari kama vile nyumba,magari na vito mbali mbali.

Wapenzi hao huzawadiana haswa siku zao za kumbukumbu.

Bahati amekuwa akiwapa wanaume wengine walio kwenye ndoa changamoto kuwazawadi wake zao.