Meneja wa Diamond Platnumz, Sallam SK agura Wasafi

Inadaiwa kuwa Sallam kwa sasa anafanya kazi na Harmonize.

Muhtasari

•Tetesi zinasema kwamba Sallam SK aliacha kufanya kazi na Diamond Platnumz miezi michache iliyopita.

•Sallam alisema hajawahi kuwa na tatizo na bosi huyo wa Kondegang.

Diamond Platnumz na meneja wake EL-Jeffe Mendez
Diamond Platnumz na meneja wake EL-Jeffe Mendez
Image: INSTAGRAM// SALLAM SK

Bosi wa WCB Diamond Platnumz na meneja wake Sallam SK Mendez wanadaiwa kutofautiana.

Tetesi zinasema kwamba Sallam SK aliacha kufanya kazi na Diamond miezi michache iliyopita.

Mashabiki waligundua kuwa meneja huyo haandamani tena na Diamond Platnumz kwenye ziara zake kama ilivyokuwa awali.

Sallam pia hajatoa taarifa zozote kuhusu staa huyo wa Bongo katika siku za hivi majuzi kama alivyokuwa akifanya hapo awali..

Kwa mujibu wa blogu za Tanzania, Sallam kwa sasa anafanya kazi kwa karibu na aliyekuwa msanii wa Diamond, Harmonize baada ya kuonekana kwenye moja ya show za hivi karibuni za mwanzilishi huyo wa Konde Music Worldwide.

"Kama kweli ni meneja, mbona hajaongozana na Diamond kwenye show zake za hivi karibuni? Badala yake ameenda kwenye show ya Harmonize ambaye ana beef na Diamond. Unganisha dots," blogu moja ya Tanzania ilisema.

Miaka michache iliyopita, Sallam alibainisha kuwa hana ugomvi na Harmonize baada ya kumpuuza wakati wa mazishi ya mke wa Babu Tale.

Sallam alisema hajawahi kuwa na tatizo na bosi huyo wa Kondegang.