Video ya Diamond akimsaliti Zuchu kimapenzi yaibuka huku wakithibitisha kutengana

Wawili hao wanadaiwa kutengana baada ya Diamond kumsaliti Zuchu kimapenzi.

Muhtasari

•Imeibuka video ya Diamond akimpiga busu mwanamke mmoja ambaye hajatambulika katika eneo moja la burudani  jijini London, Uingereza.

•Diamond alibainisha kuwa yeye na Zuchu wamebaki kuwa kaka na dada baada ya kila mmoja kuenda njia tofauti.

aonekana akimbusu mwanamke mwingine nchini Uingereza.
Diamond aonekana akimbusu mwanamke mwingine nchini Uingereza.
Image: HISANI

Vidokezo vingi kuwa mwimbaji Diamond Platnumz alimsaliti Zuchu kimapenzi na kusababisha kutengana kwao vimeendelea kuibuka.

Huku wawili hao wakiaminika kuwa kwenye mzozo wa mapenzi, imeibuka video ya bosi huyo wa WCB akimpiga busu mwanamke mmoja ambaye hajatambulika katika eneo moja la burudani  jijini London, Uingereza.

Staa huyo wa Bongo alikuwa ameenda kujivinjari katika kilabu usiku wa Ijumaa baada ya kuhudhuria tamasha kubwa la Chris Brown wakati mtu mmoja alimrekodi  akifurahia muda na mwanadada huyo  na hata kumbusu. Wawili hao walionekana kufahamiana vizuri na wenye furaha pamoja.

Madai yameibuka kwamba tukio hilo ni mojawapo ya sababu ya ugomvi wake na Zuchu ambao ulipelekea kuvunjika kwa mahusiano yao.

Diamond  alithibitisha kuvunjika kwa mahusiano yake na bintiye Khadija Kopa siku ya Jumamosi baada ya wawili hao awali kuonyesha vidokezo kadhaa kwamba uhusiano kati yao umeingiwa na dosari.

Katika taarifa yake ya Jumamosi jion kwenye  Instagram, staa huyo wa Bongo aliweka wazi kwamba yeye na Zuchu sio wapenzi tena.

Diamond alibainisha kuwa yeye na msanii huyo wake wamebaki kuwa kaka na dada licha ya awali kuonyesha mahaba makubwa yasiyovunjika kati yao.

"Kwa pamoja na Zuhura tunaomba tuwataarifu ya kwamba, kwa sasa sisi ni dada na kaka na si wapenzi kama ilivyokuwa ikidhaniwa ama wengine kujua.. Mnaruhusiwa wachumba na wake ama waume kama tutawaridhia," alisema.

Diamond aliongeza, "Lakini muwe na vibarua vinavyoeleweka  sio mje kutuchuna, maana atuhongi hovyo."

Siku ya Ijumaa, Zuchu aliibua wasiwasi juu ya hali ya mahusiano yao kufuatia chapisho lake kwenye mtandao wa Snapchat.

Mwimbaji huyo wa kibao 'sukari' alidokeza kwamba amevunjwa moyo na mpenzi wake na kutangaza kuwa yuko single.

"Single.." aliandika na kuambatanisha na emoji ya moyo uliovunjika '💔'

Aidha, binti huyo wa Khadija Kopa pia alichukua hatua ya kufuta picha zote za bosi wake Diamond kwenye mtandao wa Instagram.

Diamond pia anadaiwa kuwa na uhusiano  wa kimapenzi na mmoja wa wafanyikazi wake katika Wasafi, Aaliyah Mohamed.